Kiongozi wa Upinzani Tunisia Azimia Gerezani Kufuatia Joto Kali la Nyuzi 52°C

Kiongozi wa Upinzani Tunisia Azimia Gerezani Kufuatia Joto Kali la Nyuzi 52°C

Kadhakan

Senior Member
Joined
Jul 20, 2026
Posts
126
Reaction score
201
Kiongozi wa upinzani nchini Tunisia,Rached Ghannouchiamepoteza fahamu kwa muda akiwa katika Gereza la Mornaguia kutokana na wimbi kali la joto linalokadiriwa kufikia nyuzi 52 za Selsiasi.
​
Screenshot_20260723-095417.png


Tukio hilo lilishuhudiwa na Haifa Chebbi, binti wa mwanasiasa wa upinzani aliyefungwa, Ahmed Nejib Chebbi, ambaye alisema baada ya kutembelea gerezani alishindwa hata kupumua vizuri na kutembea kutokana na joto kali lililokuwa ndani ya gereza.
Screenshot_20260723-095931.png


Kwa mujibu wa Haifa, wafungwa wengi hukaa kwenye vyumba vya ukubwa wa takribani mita za mraba 16 kwa muda mwingi wa siku na huruhusiwa kutoka nje kwa saa mbili pekee kila siku, hali ambayo imezidisha mateso yao wakati wa wimbi hilo la joto.

Ahmed Nejib Chebbi ni mmoja wa waanzilishi wa muungano wa upinzani wa National Salvation Front (FSN), unaopinga utawala wa Rais Kais Saied. Mwaka 2025, yeye pamoja na viongozi wengine 36 wa upinzani walihukumiwa kifungo kwa makosa ya kula njama dhidi ya usalama wa taifa.

Soma zaidi: Kiongozi wa Upinzani Tunisia Jela kifungo cha Maisha kwa kosa la kuanzisha Idara ya Usalama ya Siri

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, aliikosoa kesi hiyo akisema ilikumbwa na ukiukwaji wa haki za washtakiwa na kutoa wasiwasi kuwa huenda kulikuwa na sababu za kisiasa nyuma ya hukumu hizo.
Screenshot_20260723-100148.png


Rached Ghannouchi, ambaye aliwahi kuwa Spika wa Bunge la Tunisia na kiongozi wa chama cha Ennahda, amekuwa gerezani tangu mwaka 2023.

Mnamo Aprili 30, 2026, alipelekwa hospitalini baada ya afya yake kuzorota ghafla, lakini baadaye alirejeshwa katika Gereza la Mornaguia.

Katika video yake, Haifa Chebbi alisisitiza kuwa hakuwalaumu maafisa wa gereza kwa hali hiyo, akisema wanafanya kila wawezalo kuwahudumia wafungwa, hususan wazee ambao wanapatiwa uangalizi maalumu.

Hata hivyo, alisema tukio la Ghannouchi kupoteza fahamu linaonyesha athari kubwa za mazingira magumu ya gerezani kwa wafungwa wenye umri mkubwa, ambao baadhi yao wanakabiliwa na msimu wa nne wa joto kali wakiwa gerezani.

Haifa pia aliwataja wafungwa wengine wa kisiasa wanaoendelea kuzuiliwa, akiwemo mwanasheria Abir Moussi, mwanasheria Ayachi Hammami, mwanahabari wa redio Ziad El Hani, pamoja na mwanaharakati Chaima Issa, ambao wote ni miongoni mwa viongozi wa upinzani wanaoshikiliwa nchini humo.

Haifa Chebbi alihusisha kukamatwa kwa viongozi wa upinzani na hali ya sintofahamu inayolikumba taifa la Tunisia, ikiwemo uhaba wa maji na umeme unaoendelea kuwasumbua wananchi. Alisema changamoto hizo hazipo magerezani pekee, bali zimeenea katika jamii kwa ujumla.

Akitoa wito kwa wananchi, Haifa aliwataka Watunisia kushiriki katika kuleta mabadiliko ya kweli ya kisiasa nchini. Alisisitiza kuwa mustakabali wa taifa unategemea hatua zitakazochukuliwa na wananchi wenyewe.

"Sisi ndiyo tuna wajibu wa kila kitakachotokea, kiwe chema au kibaya," alisema Haifa, akihimiza umoja na hatua za pamoja katika kutafuta suluhisho la changamoto zinazoikabili Tunisia.

=================
An intense heatwave has worsened the already harsh conditions faced by inmates at Tunisia’s Mornaguia prison and recently caused jailed opposition leader Rached Ghannouchi to temporarily lose consciousness, according to the daughter of another prominent political prisoner who says she witnessed the incident.

Haifa Chebbi, daughter of imprisoned 81-year-old opposition politician Ahmed Nejib Chebbi, said in an emotional live video posted on Facebook after a visit to the jail on Tuesday that she saw the 85-year-old Ghannouchi faint in the stifling heat and she felt barely able “to breathe or even walk on my own feet” by the time she left.
She said the temperature inside Mornaguia prison reached 52 degrees Celsius (126 degrees Fahrenheit) during her visit. Detainees spend most of their time confined to cells no larger than 16 square metres (172 square feet), she added, and are only allowed to spend two hours a day outside.

In 2022 her father helped establish the National Salvation Front (FSN), a broad coalition of secular, liberal and Islamist groups opposed to the increasingly authoritarian rule of President Kais Saied. He was among 37 opposition figures charged with “conspiracy against state security” in 2025, and was sentenced to 12 years in jail.

United Nations human rights chief Volker Turk described the imprisonment of the 37 defendants as “a setback to justice and rule of law”.

“The process was marred by violations of fair trial and due process rights, raising serious concerns about political motivations,” Turk said in a statement in 2025.
Ghannouchi, a former parliament speaker and leader of the Ennahda political movement, has been imprisoned since 2023. He was rushed to hospital on April 30 following a sharp deterioration in his health, but is now back in Mornaguia prison.

In her video, Haifa was careful not to blame prison staff for conditions in the jail, saying they were doing everything they could and that elderly prisoners in particular were receiving special attention.

She said the incident she witnessed highlighted the toll prison conditions are taking on elderly inmates, several of whom are spending their fourth summer behind bars.

She named several other imprisoned opposition figures, including lawyers Abir Moussi and Ayachi Hammami, prominent radio journalist Ziad El Hani, and activist Chaima Issa.

Linking the detentions to wider unrest over water and electricity shortages, Haifa said the crisis extends beyond prison walls. She called on Tunisians to take action to achieve meaningful political change, saying: “We are responsible for everything that will happen, whether negative or positive.”

Source: Al-Jazeera
 
Back
Top Bottom