Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kukiwa kumebaki kilomita 200 tu msafara wa vifaru vya uasi wa Wagner mara ulisitishwa na kutolewa tangazo kuwa kiongozi wa uasi huo, Prigozhin amesitisha uasi huo na kuwataka askari wake warudi makambini mwao.
Pamoja na hivyo ikatangazwa kuwa kaika makubaliono ya Urusi na kiongozi huyo yaliyosimamiwa na kiongozi wa Belarus ni kuwa Prigozhin angehamishiwa na amekubali kwenda huko.
Rais wa Erdogan alikuwa amempigia simu awali Rais mwenzake wa Urusi muda uasi huo ulikuwa umeshika kasi kuwa atumie akili yake vizuri katika mzozo huo.Vile vile wakati msafara wa uasi ukikaribia Moscow vikosi vya askari wa Chechen walikwisha pelekwa pembezoni mwa Moscow tayari kwa mapambano na askari wa Wagner.
Pamoja na yote hayo imeelezwa kuwa tangu tamko la usitishwaji wa uasi huo na makubaliano yake kutangazwa hakujaonekana dalili yoyote ya Prigozhin kuingia Belarus na wala kupata matamshi yake anayotoa mara kwa mara kupitia ukurusa wake wa Telegram.