DOKEZO Kiongozi wa Wilaya ya Maswa anayedaiwa Kuhujumu Mafuta ya Magari ya Serikali Afichuliwa

DOKEZO Kiongozi wa Wilaya ya Maswa anayedaiwa Kuhujumu Mafuta ya Magari ya Serikali Afichuliwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Madereva wa magari ya serikali katika halmashauri ya wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, wamemlalamikia,Katibu Tawala wa wilaya(DAS)ya Maswa,Athuman Kalaghe kwa madai ya kuamrishwa kuacha sehemu ya mafuta wanayopewa kwa matumizi ya magari yao, ili kiongozi huyo ayatumie kwa matumizi binafsi.

Kwa mujibu wa madereva hao, kila wanapopewa kibali cha kuchukua mafuta kupitia kituo cha Mafuta cha Walji kilichopo mjini Maswa kwa mfano lita 30 — hupewa maelekezo yasiyo rasmi kuacha takribani lita tano, kabla ya kuondoka kituoni na utaratibu huo usimamiwa na msimamizi wa kituo hicho anayejulikana kwa jina moja maarufu la Logo.

"Mara nyingi tunaandikiwa lita 30 lakini tunaambiwa tuchukue lita 25 tu, zile tano zinazobaki kiongozi anazichukua na kuweka kwenye gari lake binafsi," alisema mmoja wa madereva.

Madereva hao wamedai kuwa mfumo huu wa hujuma umekuwa ukiendelea kwa muda mrefu, hali inayosababisha baadhi ya magari kushindwa kutekeleza majukumu kikamilifu kutokana na upungufu wa mafuta.

Utaratibu huo hufanywa na kiongozi huyo pale anapopewa jukumu la kusimamia mafuta katika shughuli mbalkimbali zikiwemo ziara za viongozi wa kitaifa wanapofika wilayani humo na hata kwenye shughuli za kitaifa zinazohusisha magari mengi zikiwemo mbio za Mwenge.

Hivi karibuni katika ziara ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara,Stephen Wassira wilayani humo na mafuta ya magari kwenda wilayani Meatu kutokea Maswa yalitolewa na serikali na masimamizi alikuwa ni yeye hivyo kila gari lilipatiwa lita 30 hivyo ilibidi yaache lita 5 na kila gari liliwekewa lita 25 badala ya lita 30 za mafuta aina ya dieseal.

Mmoja wa madereva alisema kuwa walipojaribu kulalamika kwa uongozi wa juu, waliitwa na kuonywa dhidi ya "kuvujisha siri" na kwamba hatua kali zingechukuliwa iwapo wangeendelea kulalamika.

Pia wanadai hata posho zao zinapopitia kwa kiongozi huyo wanazungushwa kupatiwa na wakipatiwa hupewa pungufu na wakiulizia kwa cashier wa halmashauri ambaye ndiye huandaa malipo hayo wanakuta ni hesabu tofauti na hata wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya baadhi yao hushindwa kuwapatia posho zao na jambo la kujiuliza kitendo cha kiongozi huyo kujigeuza Cashier wa halmashauri?

Pia hulazimisha katika vikao vya kamati ya Ulinzi na Usalama vya Wilaya chakula kipikwe katika mghahawa wake ambao uko nje ya jengo la ofisi ya Mkuu wa wilaya ambao unasimamiwa na ndugu yake aitwaye,Jamila Kalaghe na bei ambayo ameelekeza yeye huku wakiwepo watu ambao wamechaguliwa kutoa huduma serikalini ambao wanalipa kodi na mapato mengine ya serikali.

Mmoja wa Maofisa wa ofisi ya Mkaguzi wa Ndani mkoa wa Simiyu amesema vitendo vya aina hiyo ni ukiukwaji wa maadili ya utumishi wa umma na kwamba endapo taarifa hizo zitathibitika, hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa kwa kuitaarifu Mamlaka yake ya uteuzi.

"Mafuta yanatolewa kwa matumizi rasmi ya magari ya taasisi, si kwa matumizi binafsi ya mtu yeyote. Hili ni kosa kubwa," alisema
 
Back
Top Bottom