LGE2024 Kiongozi wako wa Mtaa alikuahidi nini? Je, ametimiza?

LGE2024 Kiongozi wako wa Mtaa alikuahidi nini? Je, ametimiza?

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Salam ndugu zangu,

Mwaka mwingine wa uchaguzi wa Serikali za Mtaa umefika. Ni wazi kwamba viongozi wetu tulionao walitoa ahadi mbalimbali Uchaguzi uliopita tukawaamini na kuwapa nafasi.

Vipi kiongozi wa Mtaa wako ametimiza ahadi au ndiyo atakuja kuomba nafasi nyingine?

Kwa upande wangu nimeishi mitaa mitatu mpaka sasa sijaona kabisa kazi za Viongozi wa Mitaa yote niliyokaa. Naona kama viongozi wanachukulia vyeo vyao kama title tu ya kisiasa na sio wajibu.

Vipi upande wa mtaa wako mambo yapoje? Tia neno hapa tujue.
 
Kuna mwenyeketi ukienda kwake anakuambia ujiandikie barua wewe mwenyewe maana yeye hajui kuandika inafikirisha Sana .
 
Nimesha andaa upanga wangu kwa ajili ya atakae kuja ka usiku usiku hivi kwa ajili ya kuomba uungwaji mkono kutoka kwangu hakika ataenda kuwasimulia wenzie kitakacho mpata, kupiga kura kwangu mimi ni jambo la kipumbavu tuu halina maana yoyote
 
Binti uliyemtongoza akakupa umetimiza ahadi ulizompa
 
Kwan viongoz walichaguliwa?!
Asilimi. Kubwa walipita kwa baraka za mwendazake
Kwa hiyo wanafanya kwa sababu wao ni watawala sio kama viongoz
 
Nimesha andaa upanga wangu kwa ajili ya atakae kuja ka usiku usiku hivi kwa ajili ya kuomba uungwaji mkono kutoka kwangu hakika ataenda kuwasimulia wenzie kitakacho mpata, kupiga kura kwangu mimi ni jambo la kipumbavu tuu halina maana yoyote
Sahihi kabisa, maana Tanzania hakuna uchaguzi bali Kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Back
Top Bottom