Kiongozi yeyote anayedhani bila yeye chama hakiwezi kupiga hatua huyo hafai kabisa

Kiongozi yeyote anayedhani bila yeye chama hakiwezi kupiga hatua huyo hafai kabisa

markp

Senior Member
Joined
Sep 26, 2013
Posts
194
Reaction score
327
Kama wewe ni kiongozi katika chama cha siasa au taasisi yoyote kubwa na chini yako kuna wafanyakazi wengi kufikifi kuwa bila wewe kampuni au chama kitakufa basi wewe ndio utakuwa tatizo katika hiyo taasisi.

Kiongozi mzuri ni yule anayeandaa watu kuwa viongozi anajua kuna kufa, kuugua, kustaafu nk sasa kama muda wote umekaa katika nafasi ya juu na umeshindwa kuwaandaa viongozi kila mtu humuamini wewe ni kirusi.

Mheshimiwa Mbowe na Mheshimiwa Lissu wote ni viongozi wa ngazi za juu chadema na chini yao yupo katibu na viongozi wa kanda na wanachama kwa ujumla.

Kama hawa wawili kila moja anaona bila yeye chama kitayumba au kufa basi muda wooote waliokaa kwenye chama watakuwa wametufelisha sana katika mambo mengi.

Namaliza kwa kusema uongozi ni kupewa ridhaa ya kuwaongoza watu kwa muda flani na sio kujipa ridhaa wewe mwenyewe
 
Back
Top Bottom