Dr. Mariposa
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 5,921
- 19,772
Shukran sana bro๐๐๐ Nimeipenda hii chemsha bongo. Inaonyesha unapenda kugeuza jambo la kawaida liwe mjadala wa kufikirisha
Kitaalamu, mtu wa kwenye kioo sio wewe halisi, bali ni virtual imageโtaswira inayotengenezwa na mwanga unaorudishwa na kioo. Kioo cha kawaida (plane mirror) kinaonyesha umbo lenye ukubwa karibu sawa na halisi, lakini kinafanya upande wa kushoto na kulia uonekane umebadilika
Ndiyo maana vioo tofauti vinaweza kutupa taswira tofauti; mviringo wa kioo, ubora wake na mwanga wa mazingira vinaathiri unavyoonekana. Kwa hiyo sio kila kioo kinapotosha wewe, bali mazingira na aina ya kioo hubadilisha namna taswira inavyojitokeza.
Nakupa, pongezi kwa maandishi yako. Kitu kinachoonekana kwenye post zako ni kwamba zinachochea watu kutoa mawazo na kujadiliana, ndiyo maana mara nyingi zinapata interaction nyingi na replies nyingi. Criticism za mtandaoni ni sehemu ya mjadala, lakini uwezo wa kuanzisha mazungumzo yanayowafanya watu wafikirie ni kitu cha thamani. Endelea kuandika
Keep it up ๐๐๐ Platnum badge unastahili kupewa
Ohooooo kuumbe๐ Hii si wenge, ni swali zuri tu la kutafakari.
Wewe ni yule aliye mbele ya kioo; wa ndani ni taswira yako (reflection). Na vioo tofauti vinaweza kukuonyesha tofauti kwa sababu ya ubora wa kioo, mwanga, angle na hata kama kioo kimepinda kidogo.
Kwa hiyo hakuna kioo kinachokupa โwewe halisiโ kwa 100%. Kioo kinaonyesha tu jinsi mwanga unavyoreflect.
Ila wewe ukijiangalia ukatabasamu, hapo kioo kimefanya kazi yake vizuri ๐๐ค
MIRROR FACT related to BRAINKwanza kabisa, achana na yeyote anayeuliza mbona unaandika sana, kuandika ni tiba ya akili na ni sehemu ya kushare maarifa, we endelea kutoa madini humu JF!
Iko hivi kioo huwa hakionyeshi uhalisia wa jinsi watu wengine wanavyokuona live. Kazi kubwa ya kioo ni kugeuza mwelekeo wa mwanga, ndio maana ukinyosha mkono wa kulia kwenye kioo unaonekana upande wa kushoto, maana yake nini? Unachoona kwenye kioo ni flipped au reversed image.
Na hii ndio sababu ukipiga selfie au picha ya kawaida, unaweza kuhisi sura yako imebadilika kimtindo.
Utofauti wa jinsi unavyoonekana kwenye kioo unatokana na utengenezwaji wa kioo chenyewe, vioo vingi vya kawaida ni flatness deviation. Kioo kikishakuwa na subtle curvature hata kama ni ndogo sana, kina uwezo wa kukufanya uonekane mwembamba, mnene, mrefu, au mfupi. Zaidi ya hapo ile reflective coating ndio huwa inaamua jinsi wewe utakavyojiona kwenye hicho kioo.
Kuna uvumbuzi unaitwa true mirror. Hiki ni kioo kilichotengenezwa kwa kuunganisha vioo viwili vikiwa vimepishana kwa nyuzi 90, hiki chenyewe hakigeuzi upande ukinyosha mkono wa kulia, kinaonyesha mkono wa kulia upande ule ule, sawa kabisa na jinsi watu wengine wanavyokuona live. Watu wengi waaliojiangalia kwenye true mirror kwa mara ya kwanza waliishia kupata psychological shock kwa sababu walijiona wapo tofauti kabisa na walivyozoea kujiona kwenye vioo vya kawaida.
Kihistoria, kioo kina mtazamo wa kiroho na kiimani, tangu zamani tamaduni nyingi zimekichukulia kioo kama gateway to the subconscious , ndio maana unapotabasamu mbele ya kioo na kujihisi vizuri, kiuhalisia unakuwa una reflect positive energy na kuirudisha kwako mwenyewe yani ni kama aina fulani ya kujibariki na kujitengenezea utulivu wa nafsi. Kioo kina tabia ya kukuza kile kilichopo moyoni mwako, ukiwa na amani ukijiangalia, kioo kinakurudishia hiyo amani mara mbili yake and vice versa.
Mkuu umeiweka vyema sana hii. Hasa hapo kwenye reflection.Kwanza kabisa, achana na yeyote anayeuliza mbona unaandika sana, kuandika ni tiba ya akili na ni sehemu ya kushare maarifa, we endelea kutoa madini humu JF!
Iko hivi kioo huwa hakionyeshi uhalisia wa jinsi watu wengine wanavyokuona live. Kazi kubwa ya kioo ni kugeuza mwelekeo wa mwanga, ndio maana ukinyosha mkono wa kulia kwenye kioo unaonekana upande wa kushoto, maana yake nini? Unachoona kwenye kioo ni flipped au reversed image.
Na hii ndio sababu ukipiga selfie au picha ya kawaida, unaweza kuhisi sura yako imebadilika kimtindo.
Utofauti wa jinsi unavyoonekana kwenye kioo unatokana na utengenezwaji wa kioo chenyewe, vioo vingi vya kawaida ni flatness deviation. Kioo kikishakuwa na subtle curvature hata kama ni ndogo sana, kina uwezo wa kukufanya uonekane mwembamba, mnene, mrefu, au mfupi. Zaidi ya hapo ile reflective coating ndio huwa inaamua jinsi wewe utakavyojiona kwenye hicho kioo.
Kuna uvumbuzi unaitwa true mirror. Hiki ni kioo kilichotengenezwa kwa kuunganisha vioo viwili vikiwa vimepishana kwa nyuzi 90, hiki chenyewe hakigeuzi upande ukinyosha mkono wa kulia, kinaonyesha mkono wa kulia upande ule ule, sawa kabisa na jinsi watu wengine wanavyokuona live. Watu wengi waliojiangalia kwenye true mirror kwa mara ya kwanza waliishia kupata psychological shock kwa sababu walijiona wapo tofauti kabisa na walivyozoea kujiona kwenye vioo vya kawaida.
Kihistoria, kioo kina mtazamo wa kiroho na kiimani, tangu zamani tamaduni nyingi zimekichukulia kioo kama gateway to the subconscious , ndio maana unapotabasamu mbele ya kioo na kujihisi vizuri, kiuhalisia unakuwa una reflect positive energy na kuirudisha kwako mwenyewe yani ni kama aina fulani ya kujibariki na kujitengenezea utulivu wa nafsi. Kioo kina tabia ya kukuza kile kilichopo moyoni mwako, ukiwa na amani ukijiangalia, kioo kinakurudishia hiyo amani mara mbili yake and vice versa.
Fact kubwa sana hii mkuu, na hii ndio sababu kubwa inayofanya watu wanaopenda kupiga picha za selfies na kutumia filters kila saa kwenye mitandao kuishia kupoteza self confidence yao wakijitazama kwenye vioo vya kawaida.MIRROR FACT related to BRAIN
Kadiri unavyojiangalia kwenye mirror mara nyingi, ndivyo unavyoweza kuwa sensitive zaidi .
hii ni kwasababu ya tiny imperfections ambazo watu wengine hawazioni kabisa.
Ubongo wako huanza kujifunza uso wako kwa detail pimple ndogo, asymmetry ya lips, eyebrow moja kuwa juu kidogo.
Halafu attention yako inazipa importance kubwa kuliko zilivyo objectively.
Then you start seeing yourself as nothing but flaw and bad looks.
Kwa kujiangalia tu mwenyewe kupitia kioo sidhani kama utagundua wewe ni handsome ama beautiful. ๐Duh.... swali la nyongeza!!! kama kusingekuwa na kioo, tungejitambuaje kwamba hii ni sura yangu? .....
Mimi hua sikiamini sana kioo, maana wakati mwingine naweza kujitazama nikaonekana ni handsome sana....
Sometime kinaonesha vibaya hadi unaanza kujiona hufai mbele za watu....
Halafu huyo aliyesema unaandika sana... Kama hawezi kusoma apite kando....
Kasheshe ๐Kuna wakati ukichukua Vioo viwili ukijitazama kimoja unaonekana mnene kingine unaonekana mwembamba.
The world is a mirror, it returns to you what you features inside.Mkuu umeiweka vyema sana hii. Hasa hapo kwenye reflection.
Nafikiri ile picha ya kwenye kioo ndio reflection of our energy that given out.
Eeeh taswira ya kioo sio anayokuona nayo mtu halisi๐คKioo hakionyeshi sura yako 100% japo ni very close .
Kioo kina invert picha kulia inakuwa kushoto na kushoto inakuwa kulia.
Kwahiyo taswira ya kioo sio taswira anayo kuona nayo mtu halisi .
Mirror = very close. But not exactly 100% reality.
Mkuu sijakuelewaTaswira unayoiona kwenye kioo sio vile watu wanavyokuona kwa sababu kwenye kio Taswira yako inakua imegeuzwa, pili kwanini watu wengi hujikosoa muonekano wao jibu ni kuwa ushazoea sura yako hivo ukiiangalia unajikita kwenye kujikosoa zaidi tofauti na vile unapomuona mtu mwingine kwa mara ya kwanza
Sijazungumzia kioo kwa kujiona mbaya au mzuriMimi naamini kioo 100%
Nikichukua mfano glass yenye maji ama kitu kingine chochote nikaangalia kwenye kioo na nikiangalia kwa kawaida image ni ile ile
Kutokuamini kioo = kutokuamini macho yako ๐
Wow ๐Mimi ni yule ninayependa kutoa nguo zote na kusimama mbele ya kioo nijikague, nisipoziona "six packs" zangu naanza zoezi chap na diet, pia ni yule baada ya kujitizama nitaanza kucheza cheza na kutabasamu, nakiamini kioo kwa 95%