Kioo kinatuonyesha ukweli kwa kiasi gani?

Kioo kinatuonyesha ukweli kwa kiasi gani?

Kwa kujiangalia tu mwenyewe kupitia kioo sidhani kama utagundua wewe ni handsome ama beautiful.

Ili ujue wewe ni handsome/beautiful walau watu wasiopungua kumi wakutamkie waziwazi tena wa jinsia zote.

Kama hujawahi kuambiwa na watu kuanzia kumi basi wewe upo kundi la kina Masoud Surambaya.
Hahahahahaaa ......dah ukisubiri watu wakambie mkuu, utapata stress za bure....
 
Kwanza kabisa, achana na yeyote anayeuliza mbona unaandika sana, kuandika ni tiba ya akili na ni sehemu ya kushare maarifa, we endelea kutoa madini humu JF!

Iko hivi kioo huwa hakionyeshi uhalisia wa jinsi watu wengine wanavyokuona live. Kazi kubwa ya kioo ni kugeuza mwelekeo wa mwanga, ndio maana ukinyosha mkono wa kulia kwenye kioo unaonekana upande wa kushoto, maana yake nini? Unachoona kwenye kioo ni flipped au reversed image.

Na hii ndio sababu ukipiga selfie au picha ya kawaida, unaweza kuhisi sura yako imebadilika kimtindo.

Utofauti wa jinsi unavyoonekana kwenye kioo unatokana na utengenezwaji wa kioo chenyewe, vioo vingi vya kawaida ni flatness deviation. Kioo kikishakuwa na subtle curvature hata kama ni ndogo sana, kina uwezo wa kukufanya uonekane mwembamba, mnene, mrefu, au mfupi. Zaidi ya hapo ile reflective coating ndio huwa inaamua jinsi wewe utakavyojiona kwenye hicho kioo.

Kuna uvumbuzi unaitwa true mirror. Hiki ni kioo kilichotengenezwa kwa kuunganisha vioo viwili vikiwa vimepishana kwa nyuzi 90, hiki chenyewe hakigeuzi upande ukinyosha mkono wa kulia, kinaonyesha mkono wa kulia upande ule ule, sawa kabisa na jinsi watu wengine wanavyokuona live. Watu wengi waliojiangalia kwenye true mirror kwa mara ya kwanza waliishia kupata psychological shock kwa sababu walijiona wapo tofauti kabisa na walivyozoea kujiona kwenye vioo vya kawaida.

Kihistoria, kioo kina mtazamo wa kiroho na kiimani, tangu zamani tamaduni nyingi zimekichukulia kioo kama gateway to the subconscious , ndio maana unapotabasamu mbele ya kioo na kujihisi vizuri, kiuhalisia unakuwa una reflect positive energy na kuirudisha kwako mwenyewe yani ni kama aina fulani ya kujibariki na kujitengenezea utulivu wa nafsi. Kioo kina tabia ya kukuza kile kilichopo moyoni mwako, ukiwa na amani ukijiangalia, kioo kinakurudishia hiyo amani mara mbili yake and vice versa.
Asante kwa maoni mjarabu 🔥
Umenyoosha twin 👌
Sasa nimeamua kioo changu ni wewe hapo 🤪
 
Sijazungumzia kioo kwa kujiona mbaya au mzuri
Ila je hiyo taswira yako unayoiona kwenye kioo unaamini kwa kiasi gani kama ni wewe halisi ?

Hata mie nimezungumzia hapo hapo kwenye kuamini nachoona ndiyo maana nimetolea mfano wa glass ya maji

Sijazungumzia uzuri ama ubaya
 
Mkuu maada zako ni chokozi sana. Bado nawaza nini huwa motive kwako mpaka kupata hizi maada?

Anyway binafsi nafikiri kioo kinaonesha asilimia 90-100% ya uhalisia wetu lakini pia hutegemea na aina ya kioo.

Magari yote na pikipiki hutumia kioo kuonyesha mbele, nyuma na ubavuni na ukifanya chochote kinyume na kioo matokeo yake huonekana ni mabaya. Hivyo utakubaliana namimi kwamba kioo ni halisia.

Based on hearsays: Kwamba wachawi nao hutumia kioo kufanya mambo yao. Waganga nao hutumia kioo kupiga ramli.

Hivyo naweza kuhitimisha kwa kusema kioo huonyesha uhalisia wa kitu/mtu.

Binafsi sipendi kioo, at some point naweza kusema nakichukia tuu ila sina sababu za msingi. Hii kukichukia ilichagizwa na mazingira fulani

Nilikuwa naishi Mbezi Goigi, jamaa tuliyepanga nae akaingia chumbani kwangu akaona Sina kioo nayeye alikua navyo viwili akanipa kimoja pasipo kumuomba. Aisee kile kioo kilikua na maajabu mwisho wa siku nilikivunja akaishia kunikasirikia.

Toka hapo sioipendi zaidi kioo, nikipita sehemu inakioo huwa nakwepa kabisa kujiangalia. Kama ninahaja ya kujiangalia bhasi huwa natumia kioo cha simu.
Aisee pole sana mkuu
So umepoteza ujasiri wa kujiangalia ?

Hivi kuna uchawi wa kioo au ni fix?
 
Kwa kujiangalia tu mwenyewe kupitia kioo sidhani kama utagundua wewe ni handsome ama beautiful. 😄

Ili ujue wewe ni handsome/beautiful walau watu wasiopungua kumi wakutamkie waziwazi tena wa jinsia zote.😄

Kama hujawahi kuambiwa na watu kuanzia kumi basi wewe upo kundi la kina Masoud Surambaya.😄
Masoud Surambaya why Masudiii?
Hivi wanaume nao hua mnasifiana uzuri?
 
So umepoteza ujasiri wa kujiangalia ?
Hapana sijapoteza ujasiri.

Nilikua sipendi kujiangalia lakini kutokana na hilo ndio nikapata sababu ya kutokujiangalia.

Hivi kuna uchawi wa kioo au ni fix?
Hakuna UCHAWI wa kioo ila wanaofanya UCHAWI wanaweza kutumia kioo. Based on hearsays na kile nilichokiona kwangu.
 
Kioo huwa kinadanganya ubongo!!
Mf : hufanya mtu ajione mzuri mara Tano zaidi ya alivyo ili kubust confidence

Kwahyo ulivyo kwenye kioo toa mara Tano ya sura yako ndo ulivyo in reality, ukiongeza make up kwa (Ke) toa mara kumi ndo watu tunavokuona
Hivyo vipimo vyako ni kwa mjibu wa utafiti?
 
Hapana sijapoteza ujasiri.

Nilikua sipendi kujiangalia lakini kutokana na hilo ndio nikapata sababu ya kutokujiangalia.


Hakuna UCHAWI wa kioo ila wanaofanya UCHAWI wanaweza kutumia kioo. Based on hearsays na kile nilichokiona kwangu.
So unaamini uchawi unaweza kutumika na kioo?
Nini kilitokea ?
Unaweza ku share?
 
Mimi nakuona huandiki tu ila una kitu fulani cha pekee sana katika uandishi wako. Ni uandishi wenye kufikirisha sana na akili kubwa ya reasoning ndo inaweza kuyaona unayoyaandika.
Shukran sana mkuu 😊
Karibu ndani ya mada

Unakiamini kioo chako?
 
Back
Top Bottom