Kioo kujishusha

Kioo kujishusha

ankol

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2012
Posts
2,355
Reaction score
4,260
Habari zenu wadau,
Gari yangu baada ya kutoka kwa fundi maiko nimegundua kwamba nikipandisha kioo cha upande wa dereva kikifika juu hujishusha kama robo hivi. mpaka ufanye timing ya kupandisha kidogo jidogo.
Nilipomrudia kanipa stori nyingii ikiwamo gari kupoteza kumbukumbu. akanihakikishia nitumie tu kitakua sawa. leo ninavyoandika ni mwezi sasa shida iko pale pale.
Yaani ukipandisha kinapanda mpaka mwisho then kinajishusha kidogo.
Tatizo huenda likawa nini tafadhali?
 
Nadhani vioo vya gari vyako ni All auto AU cha dereva ndio auto. Vioo vya auto huna haja ya kushikilia switch ili kipande mpaka juu. Vinakuwa na ngazi mbili, ya kupandisha kawaida na kupandisha automatically.
Sasa hivi vioo vilitengenezwa hivyo ili kuepuka kubana vidole, mkono au chochote kinachoweza kupelekea either kumuumiza mtu au kuvunja kioo. Hivyo sasa huwa vikiona kuna kikwazo kwenye upandaji wake vinajishusha vyenyewe.
Safisha rubber ya kioo na kama una mafuta ya kuspray kama wd40 pulizia kwenye ule ufito wa reli ya rubber kwenye kioo na hili tatizo litaisha kabisa.
Karibu
 
Asante, ni kweli kioo cha dereva ni auto, yaani ukipress up kinapanda moja kwa moja mpaka mwisho. Je Mafuta hayo yanauzwa sh ngapi? kuna haja ya kufungua cover la mlango kwa ndani ili ni spray hayo mafuta ama naweza spray kupitia kingo za kioo? Ahsante.
 
Habari zenu wadau,
Gari yangu baada ya kutoka kwa fundi maiko nimegundua kwamba nikipandisha kioo cha upande wa dereva kikifika juu hujishusha kama robo hivi. mpaka ufanye timing ya kupandisha kidogo jidogo.
Nilipomrudia kanipa stori nyingii ikiwamo gari kupoteza kumbukumbu. akanihakikishia nitumie tu kitakua sawa. leo ninavyoandika ni mwezi sasa shida iko pale pale.
Yaani ukipandisha kinapanda mpaka mwisho then kinajishusha kidogo.
Tatizo huenda likawa nini tafadhali?
Kipige nyundo kitaacha ujinga.
 
Asante, ni kweli kioo cha dereva ni auto, yaani ukipress up kinapanda moja kwa moja mpaka mwisho. Je Mafuta hayo yanauzwa sh ngapi? kuna haja ya kufungua cover la mlango kwa ndani ili ni spray hayo mafuta ama naweza spray kupitia kingo za kioo? Ahsante.
Mafuta yanauzwa kuanzia shilingi elfu tano 5,000 tsh. Au juu jidogo inategemea na unaponunulia..
Hapana, huna haja ya kufungua milango, pulizia kwenye reli ya plastiki kioo kinapopita ili kupanda au kushuka.
Puliza kwenye vioo vyote utaona mabadiliko makubwa sana. Na pia itaokoa motor zako za vioo zidumu kwa maana hazitakuwa zinatumia nguvu nyingi kupambana na msuguano wa kioo na kingo.
 
Back
Top Bottom