Kipa Mbeya City Asimamishwa

Kipa Mbeya City Asimamishwa

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
DAVID BURHAN ASIMAMISHWA NA KUONDOLEWA KIKOSINI.

Halmashauri ya jiji la Mbeya ambayo ndio mmiliki wa timu ya Mbeya City football Club ilikutana na bodi ya Michezo ya jiji inayosimamia uendeshaji wa timu leo tarehe 23.02.2015 kujadili muenendo mzima wa mchezo wa timu yetu dhidi ya Young African uliochezwa tarehe 22.02.2015 pamoja na
matokeo yake.

Katika kikao hicho,mmiliki pamoja na bodi yake walipitia taarifa na rejea ya mchezo husika na
kugundua mambo yafuatayo:

1. Kiufundi timu ilicheza vizuri na kwa kiwango cha hali ya juu ikilinganishwa na wapinzani wetu, ila ilikosa kitu kimoja tu nacho ni ushindi.

2. Mchezaji David Abdallah Buruhani ambaye alikuwa golikipa katika mchezo huo alifanya makosa binafsi na ya makusudi yaliyoigharimu timu kukosa ushindi katika mchezo husika.

Makosa ya mchezaji huyu katika mchezo huo yalikuwa yanafanana na baadhi ya makosa ambayo alishawahi kuyafanya huko nyuma na kusahihishwa.

Baada ya kupitia rejea kadhaa ilibainika kuwa makosa mengi ya aina hii yamekuwa yakifanyika katika baadhi ya mechi hasa zinazohusisha timu zenye ushawishi

Mazingira mazima ya makosa yote hayo yamezingirwa na mashaka makubwa ambayo ni vigumu kujiweka mbali nayo akiwa kama mhusika mkuu.

Baada ya uchambuzi wa nyaraka mbalimbali na rejea zake, mmiliki ambaye pia muajiri wa mchezaji husika amemsimamisha na kumuondoa kikosini mpaka hapo atakapomjulisha vinginevyo.

Halmashauri ya jiji la Mbeya imesikitishwa na mazingira mazima yaliyojitokeza ya kupoteza mchezo huo.

Ni kweli mchezo wa mpira wa miguu ni mchezo wa makosa ila aina gani na mazingira yapi ya kosa husika ni changamoto na kushinda na kushindwa ni sehemu ya mchezo ila umeshindwa je na katika mazingira yapi ni changamoto kubwa zaidi.

Dismas Ten
(signed)


Chanzo: Mbeya City FC
 
Tena wamtimue kabisa...pumba.vu sana kamzawadia ngasa goli la wazi kabisa...
 
Wasipoangalia watashuka daraja na ndugu zao Prison
 
Kipa hana kosa, mabeki walikuwa wapi wasimzuie ngasa? washambuliaji wamepoteza nafasi nyingi hao wamechukuliwa hatua gani? Kimsingi timu nzima ya mbeya city ni mbovu .
 
Kipa hana kosa, mabeki walikuwa wapi wasimzuie ngasa? washambuliaji wamepoteza nafasi nyingi hao wamechukuliwa hatua gani? Kimsingi timu nzima ya mbeya city ni mbovu .

Nashangaa wanaliona la ngassa vipi walipoifunga timu yenye ushawishi pia ya simba mliwapa nini cha ziada
 
..duh! togwa limeshaingiliwa na nzi, sasa waamue wenyewe kulinywa ama kulimwaga! sie twacheka tu huku twaongoza ligi! YANGA MBELE DAIMA!
 
Tatizo yanga ni hongo sana,mnaohonga wachezaji wa timu pinzani sana..ona sasa dogo mshamuharibia maisha yake,sijui hyo. M mlompa itamsaidia nn,..
 
Tena wamtimue kabisa...pumba.vu sana kamzawadia ngasa goli la wazi kabisa...

Nawashauri Polisi Morogoro nao wamtimue yule kipa aliyepiga hewa, mpira ukatinga wavuni wakati wa mechi dhidi ya Simba Mji Kasoro Bahari.

Young Africans SC is the prevailing wind that exposes the chicken's anus.

Kwa Yanga ya sasa watafukuzwa wengi mno!
 
Na Arudi akacheze ndondo. wachezaji wetu hawaangalii mbele wanatamaa za haraka haraka.Haya sasa tuone hiyo fedha aliyopewa na yanga itamfikisha wapi.
Hongera Uongozi wa mbeya city.Wengine wafuate.
 
Kaseja alifungwa goli na awadh juma ingekuwa sio kanjibai kumkingia kifua wangemtoa macho. Au mshasahau?
 
Nawashauri Polisi Morogoro nao wamtimue yule kipa aliyepiga hewa, mpira ukatinga wavuni wakati wa mechi dhidi ya Simba Mji Kasoro Bahari.

Young Africans SC is the prevailing wind that exposes the chicken's anus.

Kwa Yanga ya sasa watafukuzwa wengi mno!

Wasimfanye mbuzi wa kafara...
 
Na Arudi akacheze ndondo. wachezaji wetu hawaangalii mbele wanatamaa za haraka haraka.Haya sasa tuone hiyo fedha aliyopewa na yanga itamfikisha wapi.
Hongera Uongozi wa mbeya city.Wengine wafuate.

Hiyo siasa tu, kufungwa kafungwa kihalali, ni vp Mbeya City alalamike kwa kufungwa na Yanga?Yeye ana mpira gani wa ajabu?Alifungwa Mtibwa na Coastal kwao sembuse MC?
 
Mpira wa bongo ni kichefu chefu sana!

Kila keeper duniani kwa wakat tofaut ashawahi kufanya makosa kama hayo!!! na ndo Soccer lilivyo!

Kina Joe Hart, Casillas, Mignolet, Speron etc...washafanya hayo makosa, lakin hatujawah kusikia wakiambiwa wameuza Mechi..

Beki wa Leceister City, Morgan, kila leo anatoa maboko, lakin hatujawah kuskia akiambiwa anauza match...mpira ni mchezo wa makosa bhana na Goal ndo adhabu yenyewe..
 
Wamesahau hata cassilas wa spain alishawahi kufanya makosa kama yale kwenye world cup ya kule brazil sembesu burhan wa bongo!!!!! Mbeya city inaelekea kubaya, hasa baada ya kuchanganya mpira na siasa. Mbona hakufungiwa game na azam ambayo alifungwa goli la kizembe aje kutimuliwa leo?
 
tulipotoka sare na simba 3-3 2012 Bathezi alikumbwa na mkasa kama huu,leo kipa wa mbeya city kasimamishwa,,,,,chezeni mpira bado marudiano dar itakuwa 4-0 mtafukuza mpaka kocha
 
Fungu la usajili linahitajika kuongezwa kama mkisalia Lugi kuu msimu huu...kumbuken mlimfukuza team captain wenu na aliwasaidia sana leo kipa karibu na wale wanaoongoza kukosa mabao nao mtawatimua...kumbuken mwadui na wanalizombe nao washapata nafas hiyo mnayoichezea....chukuen hatua haraka za kiutendaji sio mchezaji
 
Back
Top Bottom