Kipa wa Cape Verde, Vozinha (40), afanya 'saves' 7 na kuipa sare timu yake dhidi ya Uhispania

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Kipa mkongwe wa Cape Verde, Vozinha (40), aliokoa michomo 7, ikiwemo 6 ya ndani ya boksi, na kuwa shujaa na kuisaidia timu yake kutoka sare ya 0-0 dhidi ya mabingwa wa Ulaya, Uhispania, katika mchezo wa Kundi H wa Kombe la Dunia 2026. Matokeo hayo yameifanya Cape Verde kupata pointi yake ya kwanza kabisa katika historia ya kushiriki Kombe la Dunia.

1781550336508.png
Uhispania ilitawala mchezo kwa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga, lakini Vozinha alikuwa imara langoni kuanzia dakika za mwanzo hadi mwisho. Aliokoa hatari kutoka kwa Pedri, Ferran Torres, Mikel Oyarzabal na Aymeric Laporte, huku Torres akigonga mwamba wa juu katika moja ya nafasi bora zaidi za Uhispania.

1781550236516.png
Mbali na kuipa Cape Verde matokeo ya kihistoria, Vozinha ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi—miaka 40 na siku 12, kucheza mechi yake ya kwanza ya Kombe la Dunia akiwa na timu ya taifa.

Vozinha anakuwa Kipa wa pili kuokoa michomo mingi baada ya Patrick Beach wa Australia anayeongoza Kombe la Dunia la FIFA 2026 kwa jumla ya mashuti yaliyookolewa, Nane katika mechi moja ya hatua ya makundi dhidi ya Türkiye.

1781551307794.png

Baada ya filimbi ya mwisho, kipa huyo alibubujikwa na machozi kufuatia kiwango chake bora na mafanikio ya kuiwezesha Cape Verde kupata pointi yake ya kwanza kabisa katika historia ya michuano hiyo.

Kufuatia kufanya maajabu hayo dhidi ya Uhispania katika Kombe la Dunia la FIFA 2026, kipa wa Cape Verde, Vozinha, ameibua gumzo kubwa duniani baada ya idadi ya wafuasi wake kwenye Instagram kupanda kwa kasi kutoka takriban 20,000 hadi zaidi ya milioni 2.7 ndani ya muda mfupi.

Vozinha JF 2.png

Miaka minne iliyopita, Uhispania ilianza kampeni yake ya Kombe la Dunia nchini Qatar kwa kuichapa Costa Rica mabao 7-0. Baada ya droo ya mashindano ya mwaka huu kuwaweka dhidi ya Cape Verde, taifa lililokuwa likishiriki Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza, wengi walitarajia matokeo ya aina hiyo kujirudia.

SnapInsta.to_724004975_18602341093061984_4180810633211783388_n.jpg
Vozinha anacheza soka la kulipwa katika Ligi Daraja la Pili nchini Ureno akiwa na G.D. Chaves. Ingawa huu ulikuwa mtihani mkubwa zaidi kwake na kwa taifa lake kutokana na ubora wa wapinzani wao, rekodi ya Cape Verde katika hatua za kufuzu ilikuwa ishara kwamba mechi hiyo isingekuwa rahisi kwa Uhispania.

SnapInsta.to_719548405_18602341075061984_5247505221202552780_n.jpg
Vozinha amecheza katika kila mechi ya kampeni ya kufuzu ya Cape Verde, ambapo aliruhusu mabao nane pekee katika michezo 10. Mabao manne kati ya hayo yalifungwa katika mechi moja dhidi ya Cameroon, huku kipa huyo akitunza clean sheet saba, zikiwemo mechi zote tano za nyumbani.

FOLLOWERS.jpg
 
Nyakati za Maximo Taifa Stars iliwahi kushinda game dhidi ya hawa Cabo Verde. Enzi hizo Tanzania ilikuwa level moja na wao kwenye soccer ila kwa sasa tofauti ni Mbingu na Nchi. Sasa hivi wenzetu wanashiriki kombe la Dunia wana anza dhidi ya bingwa wa Ulaya na wanaondoka na point.
 
Kipa mkongwe wa Cape Verde, Vozinha (40), aliokoa michomo 7, ikiwemo 6 ya ndani ya boksi, na kuwa shujaa na kuisaidia timu yake kutoka sare ya 0-0 dhidi ya mabingwa wa Ulaya, Uhispania, katika mchezo wa Kundi H wa Kombe la Dunia 2026. Matokeo hayo yameifanya Cape Verde kupata pointi yake ya kwanza kabisa katika historia ya kushiriki Kombe la Dunia.

Uhispania ilitawala mchezo kwa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga, lakini Vozinha alikuwa imara langoni kuanzia dakika za mwanzo hadi mwisho. Aliokoa hatari kutoka kwa Pedri, Ferran Torres, Mikel Oyarzabal na Aymeric Laporte, huku Torres akigonga mwamba wa juu katika moja ya nafasi bora zaidi za Uhispania.

Mbali na kuipa Cape Verde matokeo ya kihistoria, Vozinha ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi—miaka 40 na siku 12, kucheza mechi yake ya kwanza ya Kombe la Dunia akiwa na timu ya taifa.

Vozinha anakuwa Kipa wa pili kuokoa michomo mingi baada ya Patrick Beach wa Australia anayeongoza Kombe la Dunia la FIFA 2026 kwa jumla ya mashuti yaliyookolewa, Nane katika mechi moja ya hatua ya makundi dhidi ya Türkiye.

Baada ya filimbi ya mwisho, kipa huyo alibubujikwa na machozi kufuatia kiwango chake bora na mafanikio ya kuiwezesha Cape Verde kupata pointi yake ya kwanza kabisa katika historia ya michuano hiyo.

Kufuatia kufanya maajabu hayo dhidi ya Uhispania katika Kombe la Dunia la FIFA 2026, kipa wa Cape Verde, Vozinha, ameibua gumzo kubwa duniani baada ya idadi ya wafuasi wake kwenye Instagram kupanda kwa kasi kutoka takriban 20,000 hadi zaidi ya milioni 2.7 ndani ya muda mfupi.

Miaka minne iliyopita, Uhispania ilianza kampeni yake ya Kombe la Dunia nchini Qatar kwa kuichapa Costa Rica mabao 7-0. Baada ya droo ya mashindano ya mwaka huu kuwaweka dhidi ya Cape Verde, taifa lililokuwa likishiriki Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza, wengi walitarajia matokeo ya aina hiyo kujirudia.

Vozinha anacheza soka la kulipwa katika Ligi Daraja la Pili nchini Ureno akiwa na G.D. Chaves. Ingawa huu ulikuwa mtihani mkubwa zaidi kwake na kwa taifa lake kutokana na ubora wa wapinzani wao, rekodi ya Cape Verde katika hatua za kufuzu ilikuwa ishara kwamba mechi hiyo isingekuwa rahisi kwa Uhispania.

Vozinha amecheza katika kila mechi ya kampeni ya kufuzu ya Cape Verde, ambapo aliruhusu mabao nane pekee katika michezo 10. Mabao manne kati ya hayo yalifungwa katika mechi moja dhidi ya Cameroon, huku kipa huyo akitunza clean sheet saba, zikiwemo mechi zote tano za nyumbani.

Nyongeza

View: https://youtu.be/_lGmi17mRYI
 
Hawa jamaa wako wachache sana ila wanapiga mpira mkubwa sana

Tanzania tuko milioni 70 watu wajevimba matumbo kwa kula ugali machakula yasiyo na virutubisho

Ni wakati wa Zanzibar kutoka kwenye huu uvamivi unaoitwa muungano. Wenzetu walijikwamua kutoka kwenye Huo muungano wao wa kinafiki Kama wetu na Guinea Bissau , Leo wako mbali sana
 
Back
Top Bottom