Kipa wa Cape Verde, Vozinha (40), afanya 'saves' 7 na kuipa sare timu yake dhidi ya Uhispania

Kipa wa Cape Verde, Vozinha (40), afanya 'saves' 7 na kuipa sare timu yake dhidi ya Uhispania

Huyu kipa kafanya Spain aondolewe kwenye ya kwanza.. Pamoja na yote ila Spain yenyewe hata haionekani kama wanadalili za kuwa Bingwa kwa kweli...

1781610102555.png
 
Hawa jamaa wako wachache sana ila wanapiga mpira mkubwa sana

Tanzania tuko milioni 70 watu wajevimba matumbo kwa kula ugali machakula yasiyo na virutubisho
Wakienda kushangalia badala ya kuwataja wachezaji wana namna zao za kutaja watu wap wanaowajua..unategemea nini😀😀
 
Hawa jamaa wako wachache sana ila wanapiga mpira mkubwa sana

Tanzania tuko milioni 70 watu wajevimba matumbo kwa kula ugali machakula yasiyo na virutubisho
Na mkuu ujue sio kwamba watu hawapo..wapo madogo wanaupiga mwingi sana..sisi Bongo hapa unafiki na maendeleo ni pro max in madness way.

Hawa wachache waliotoka nje ya mfumo wa kimechezo wa Bongo wameteseka sana sana..wacha watu wajilie Ugali na kujaza matumbo...kuna kijitabaka flani hapa kinarudisha sana watu Nyuma kimechezo..utasikia bila yule hupiti kokote..bila Simba..bila Yanga..bila matako ya flani hatuendi..
 
Ndio ujue hapa kwetu tunakazana tu akina Lisu. Tunaacha vitu vya msingi kukuza vipaji. Fikiria miaka kadhaa tu hapo nyuma hawa Cape Verde tulikuwa tunawagonga nje-ndani. Lakini wametuacha mkiani.
Sisi kazi yetu kuzisema team za watu..ooh wale wataliwa😀😀
 
Ni wakati wa Zanzibar kutoka kwenye huu uvamivi unaoitwa muungano. Wenzetu walijikwamua kutoka kwenye Huo muungano wao wa kinafiki Kama wetu na Guinea Bissau , Leo wako mbali sana
mbona zanzibar wanapambania kupata uanachama FIFA, wapewe tu
 
Hawa jamaa wako wachache sana ila wanapiga mpira mkubwa sana

Tanzania tuko milioni 70 watu wajevimba matumbo kwa kula ugali machakula yasiyo na virutubisho
Ila ugali siyo chakula basi tu mazingira, mazoea na makuzi tuliyokulia yanatufanya tushindwe kuuacha 🤣 binafsi Huwa najipiga Marufuku kula ugali Kwa muda Fulani, ila nikishinda nyumbani basi nanunua samaki wa kukaanga na kitu Cha haraka naona nipike na ugali 🤣
 
Gatuso aende kufanya uvuvi sasa hivi atakuwa kapata jibu kwanini idadi ya timu zimwongezeka Africa.
Kuna yule beki wa zamani wa Liverpool ambaye wakati anacheza alikuwa mchezaji wa kawaida ila sasa kawa mchambuzi na kuponda wachezaji wengine na kuponda Afcon. Sasa hivi atakuwa anaona aibu, Jammie Caragher.
 
Back
Top Bottom