Corticopontine
JF-Expert Member
- Sep 20, 2019
- 666
- 1,277
PICHA: Kazi za ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Morogoro – Makutupora, Dodoma (KM 422) zinaendelea ambapo Ujenzi wa kipande hicho umefikia 61%.
Ujenzi wa Reli hiyo ya Kisasa unatarajiwa kuwekwa mifumo ya kisasa ambayo itamdhibiti mwendeshaji wa Treni kutovuka spidi iliyowekwa.
====
IMEELEZWA kuwa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), unatarajiwa kuwekwa mifumo ya kisasa ambayo itasaidia kuzuia ajali ambazo zinaweza kujitokeza wakati wa uendeshaji wa reli hiyo na ambao hautamruhusu dereva kuzidi ama kupunguza mwendo uliowekwa.
Hayo yamesemwa na Meneja Msaidizi wa mradi wa reli ya Kisasa, kipande cha Morogoro - Makutopora (Km 422) kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Christopher Mang’wela, wakati akizungumza na wahandisi kutoka Serikalini na Sekta Binafsi ambao wametembelea mradi huo uliofika asilimia 61, jijini Dodoma, kwa ajili ya kujifunza utekelezaji wa mradi kuanzia hatua mbalimbali zilizotekelezwa.
“Kama mnavyoona, mradi umefika asilimia 61, na uendeshaji wake utakuwa ni wa kisasa kwani utawekwa vifaa maalum vya kumuongoza dereva wa treni ili kuzuia ajali.” amesema Mhandisi Mang'wela.
Awali, akizungumza kwa niaba ya wahandisi hao, Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Mhandisi Patrick Barozi, ameeleza kuwa anaona nia ipo na uwezo kwa watanzania katika kusimamia miradi mikubwa inayoendelea nchini huku tukiwa na usimamizi mdogo kutoka wenzetu wa nje na hivyo kuwaleta wahandisi wetu katika mradi kutaongeza chachu ya kuchukua zabuni nyingi za miradi mikubwa inayoatarajiwa kuanza na kuendelea hapa nchini.
"Tumetembelea mradi huu katika baadhi ya maeneo ambapo tumeridhishwa na mradi huu na tumeona unaendeshwa vizuri kuanzia mwanzoni hadi hapa ulipofika kwani kupitia mradi huu wahandisi wamejifunza mengi", amefafanua Mhandisi Barozi.