Watu wengi hata kuoga hawajui ukumbuke na kuswaki ndio kabisa, mtu anaoga hasafishi tundu za pua, katikati ya vidole vya miguu hagusi, pumbu hasafishi, katikati ya mapaja ndio anapapita kama kituo cha polisi, hapo anaoga dakika moja ashatoka, ataacha kunuka huyo? Haya kuswaki unakuta mtu anapiga dry yaani kinywa hagusi ulimi, kuta ya juu na chini halafu hasuuzi kinywa na maji na mswaki ili kuondoa shombo ya dawa ya meno unakuta unaongea na mtu ananuka whitedent muda wote au micolgate, hayuko current kujua kuna dawa nyingine kama dabuur au closeup au sensodyne, hajui shaver hata za buku anyoe nywele binafsi, hajui walau kumuona dentist walau asafishe kinywa mara mbili kwa mwaka, halafu ukikuta mtu anajifanya kutoa hoja unamcheki unaona huyu basi tu wengine wasomi watu wazima kabisa .