Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Huu ndio ukweli uliopo. Nafasi uliyonayo kwa sasa au nyanja yako ya kiuchumi uliyonayo ndiyo itakayokupatia mpenzi anayeendana na hali uliyonayo. Kama hali uliyonayo itabadilika huko mbeleni, pia na uhusiano utatikisika kwa sababu utakuwa uko daraja lingine la kukutana na wenye hilo daraja. Kama hukuweka misingi imara huko nyuma, mabadiliko lazima yataathiri uhusiano...ndio maana migogoro ya kimahusiano hutokea mara kwa mara. Na mara nyingi inakuwa hivi; uchumi wa mwanaume ukishuka...bibie lazima asumbue, na uchumi wa mwanaume ukipanda lazima kidume asumbue. Hiyo ndio asili ya mwanadamu.
Note: Uliyenaye ni kutokana na daraja la uchumi au wadhiwa ulionao.
Note: Uliyenaye ni kutokana na daraja la uchumi au wadhiwa ulionao.