Kipengere cha Measure kwenye SPSS kina umuhimu mkubwa sana!!.

Kipengere cha Measure kwenye SPSS kina umuhimu mkubwa sana!!.

FestoKaguo

Senior Member
Joined
Apr 1, 2022
Posts
128
Reaction score
202
Jumatatu yangu leo nikasema nisettle nifanye coding ya data za research kwa kutumia SPSS...sasa ile wakati najaza nikafika kwenye kipengele cha Measure kama unavyoona kwenye picha hapo aisee!"

Ndipo nagundua kumbe Nominal, Ordinal, na Scale kila moja inamaana yake yaani kiufupi zenyewe si kwamba namba za kawaida tu. Ukizitumia vibaya, unaweza kuishia kupata wrong answers wakati wa ku-analyse data.

Angalia picha kwa umakini hapo kuna sehemu nimejaza Scale, Nominal na Ordinal ila sasa kila moja imejazwa hivyo for a reason haijajikalia kama kituko

Ukiangalia nominal nimeijaza sehemu yenye majina tu hapo mfano gender (1 = Male, 2 = Female)
SPSS.png


Ordinal nimeijaza sehemu inayoonesha a certain rank ( utofauti wa madaraja au ranks) Mfano job position inaonesha utofauti wa rank kati ya HR na mfanyakazi wa kawaida

Na scale yenyewe inaonesha namba zenye maana halisi Mfano age kwa sababu mtu anaweza kuwa na miaka 23.7 na ukifanya vipimo unaweza kupata mean, standard deviation, nk.


Nimejaza age kama scale kwa sababu inahusisha namba kamili zenye maana. Kwingine, kama job position au education level, nimejaza ordinal kwa sababu zinaonyesha mpangilio. Na kwenye gender, nikaweka nominal kwa sababu zenyewe zinaonesha makundi tu, hakuna level ya juu wala cha chini.

Unatumiaje measure kwenye SPSS?
Je, kuna sehemu uliwahi kutumia vibaya na kuathiri interpretation ya data zako?

Comment below au DM kama ungependa materials/short training kuhusu SPSS data coding na tufanye research iwe tamu kwako no stress amigo!!🖖
 
Mi ndio kwanza naanza kujitrain SPSS.
Hata hivyo ongera Sana bro kwa kuanzisha Uzi mzuri namna hii.
Hizi ndio nyuzi SASA
 
Mi ndio kwanza naanza kujitrain SPSS.
Hata hivyo ongera Sana bro kwa kuanzisha Uzi mzuri namna hii.
Hizi ndio nyuzi SASA
Tuko pamoja sana uzuri umepiga hatua kwa kuanza kujifunza sio mbaya mkuu
 
Transforming data chaos into breathtaking insights

We demystify data and research processes, leveraging algorithms from the deepest mathematical intricacies to handle everything from collection to analysis and reporting. Our visualizations bring even the most complex data to life. See our sample work.
chart_1.png
char_2.png
chart_2.png
chart_3.png


Your data deserves clarity. Let’s make it breathtaking.
 
Back
Top Bottom