Kipenzi changu anatishia kuondoka

Kipenzi changu anatishia kuondoka

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
25,258
Reaction score
48,589
Hello Africa

Nipo kwenye mahusiano na mdada mmoja ambaye tulijuana tukiwa shule ya upili ni mda sasa tangu tuwe kwenye mahusihano sasa kila tukigombana anakunja nguo zake anataka kuondoka na mbembeleza sasa juzi tena tumegombana kakunja nguo zake kaondoka na mimi nimemuacha sija mbembeleza kasepa zake mpaka leo sijamtafuta ila nawaza tu akirudi nimpokee au nisimpokee?
 
Mwache msichana wa watu aondoke mapema kwani kuna kila dadili za maisha kuwa magumu kwake baadaye. Tena akishafunga ndoa na wewe na kuzaa watoto ndio mambo yatamwia mabaya kabisa. Mwache aende zake!
 
We endelea kukaa kimya.

By the way;

1. Ni mkeo au mpenzi tu?
2. Unakujua alikokwenda? Au unajua ameenda kwa nani?
3. Nje ya wewe na yeye, nani mwingine anajua kuwa unaishi naye?
4. Ameondoka na chochote?

NB.
Swali langu la pili hapo juu, nimeuliza hivyo kwa sababu nina jamaa, yeye alikuwa anaishi na mwanamke kama mke na mune. Walikuwa wanaishi Dar. Mwanamke kwao Masasi. Sasa alikuwa akienda kwao anakaa muda mrefu halafu anarudi Dar. Kidogo anaanza kudai kwenda kwao Masasi...!!

Jamaa anamruhusu. Mchezo ukawa ni huo w nenda rudi. Kumbe kule Masasi ana mume mwingine. Alikuwa anaishi na wanaume wawili, Masasi na Dar. Hali iliendelea hivyo hadi mama wa mwanamke alipoona ameshindwa kutunza siri akaamua kumwambia mkwewe. WAKAACHANA.
 
Back
Top Bottom