Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
CHOJI ! Ni "smol hausi" but am on the way to be a legal couple with her ! Hata hivyo unayosema pia ni katika "maneno ya kufanyia kazi"Hii ishu inakuwa ngumu sababu huyo ni mpenzi na hatujui una malengo gani nae. Angekuwa mke/mchumba ushauri ungekua tofauti. All in all mi naona kitendo chake cha kukaa kimya mwezi mzima kinamaanisha hayuko tayari kuacha pombe, kaona bora akuache wewe!
Pole sana kwa msiba. Kuhusu mpenz wako nahc ulimtaman bila kumchunguza mwanzo. Kaanza kunywa lini? Vumilia tabia yake kwa kuwa hukutaka kumchunguza mapema! Majuto ni mjukuu.
Waungwana wadau, kwanza ninasikitika kwa kutokuepo mkekani kama ilivyo kawaida yangu kwa takriban siku 4-5 kufuatia kufiwa na Mama mdogo wangu J'2 iliopita na tumemzika jana (R.I.P mama). Wadau imefika karibu mwezi mmoja tangu nitatizane na mpenzi ambapo issue ilikua nimie kumkalia kooni aache Pombe.
Tangia hiyo siku nilimtumia msg mbili hakunijibu ambavyo si kawaida yake, kilichofata nami nikajibu mapigo ya kukaa kimya na leo imefika mwezi kamili no communication each other.
Aidha sio siri maumivu niyapatayo ni makubwa kuliko sana, yote kwa yote still bado niko na msimamo wa kutovunja ukimya kwani naamini kwa kuanza mie kuvunja ukimya ni kujirahisisha kama sio kujidhalilisha.
Nachouliza kati ya kupata hasara ya kukosa penzi na hasara ya kupata katika kazi/shughuli (kifedha) ipi yenye nafuu ?
mama mdogo!!!Kwa nini umechanga topic mbili: ya kifo cha mama (RIP mama yetu), na hiyo ya mpenzi?
Teh Sasa mbona kesi imeisha??? Mwanamke hatakiwi kuwa na kiburi cha hivyo...kumtafuta ni kujilazimisha kuingia kwenye maisha ya migogoro kila siku...huyo kimeo na si mke mtarajiwa...ni kero mtarajiwa
Tujadili topic ipi ya kufiwa au ya ukimyaa wewe na king'asti wako?
Any way R.I.P mama mdogo
Ngoja niongeze ushauri mwingine!
"huyo mwanamke mlevi na mwenye kiburi hafai kuwa mke! Hivyo tupa manyanga utafute mlokole na usijali utajifunza kumpenda tu na huyo"
Kazi ni kwako! Source Vodakomu!
Usikilize moyo wako!
Bado wamhitaji mpenzio/ana umuhimu katika maisha yako????
Kama jibu ni ndiyo, inabidi ukae nae chini uongee nae na pia unatakiwa uchukulie unywaji wake wa pombe ni sehemu ya mapungufu aliyonayo kwani kila binadamu anayo mapungufu yake.
Kwani waweza kumuacha yeye mnywaji bia na kumpata kikojozi ambapo utasikia shida zaidi.
Ngoja niongeze ushauri mwingine!
"huyo mwanamke mlevi na mwenye kiburi hafai kuwa mke! Hivyo tupa manyanga utafute mlokole na usijali utajifunza kumpenda tu na huyo"
Kazi ni kwako! Source Vodakomu!