Hili linaweza kueleweka tofauti kutokana na utofauti wa kiimani ila sahau yote zingatia hili kwanza👇
Ikiwa wewe ni Muislam!
Zingatia sana uhalali na uharamu katika utafutaji wako wa riziki!
Imekuwa ni kawaida sana kwa zama hizi kuangalia maslahi ya kidunia zaidi kuliko Akhera yetu!
Uongo, Utapeli, Riba na Kamari vimepamba moto.
Yote hayo ni kwasababu tumeyaweka mbele matamanio ya nafsi zetu kwa kuikumbatia dunia na kujisahaulisha kuhusu akhera!
KUHUSU WINGA NA UDALALI:
Kwa kweli haya mambo watu wanafanya tu ila yana taratibu zake kwa mujibu wa sheria ya kiislamu.
Sheria na taratibu hizo zinalengo la kutulinda sisi sisi, juu ya madhara ambayo hutokea pindipo watu wanapokwenda kinyume na sheria hizo!
Ilo lipo wazi, nadhani sisi wenyewe tunashuhudia matukio ya wizi, utapeli, ulaghai na kadhalika!
Yani imani imetoweka kabisa na maisha yamekuwa magumu mara dufu zaidi!
Yote hayo kwasabubu tumeyawacha mafundisho na kuzipuuza sheria na taratibu za dini ya Uislam.
Enyi Ndugu zangu katika Imani, tufahamu kwamba hayo yanahitaji mazingatio ya hali ya juu mno!
Kwa sasa sitoandika mengi sana, Ila huu ukumbusho naomba ukatufae sote, hata kwa wale wasio amini haki (Kafir) pia nao watafakari kwa kina, ili nao kwanza waje kwenye haki!
Halafu kwa pamoja tufuate muongozo sahihi!
InshaAllah Allah atufanyie Wepesi!
Naomba kwanza tusahau kuhusu hiyo post niliyopost kuhusu WINGA!
INSHAALLAH Nitaandaa post itakayoelezea namna sahihi ya kuwa Winga/Dalali mwenye mafanikio duniani na akhera, kwa kuzingatia sheria na taratibu za Uislam.