Kipi bora kati ya kuwa winga wa kila kitu au kuwa winga wa bidhaa moja tu?

wateja wenyewe hawajasoma....shule ya nini?
 
Habari zenu wakuuu..!

Hivi kipi bora kati ya kuwa winga wa kila kitu au ku-focus na bidhaa moja tu!?

Naomba maoni yenu wakuu!
Kua WINGA kwenye industry moja mfano electronics devices , clothes, plumbing, pharmaceutical, vifaa vya kilimo, vifaa vya ujenzi... N.k n.k

Too much focus na industry Zaid ya moja itakupunguzia kuielewa industry vyemaa..

So chagua industry moja weka muda na nguvu miezi sita ijayo utakua sehemu..
 
Karibuni kwa KEMIKALI NA MALIGHAFI MBALIMBALI
SULPHURIC ACID
HYDROGEN PEROXIDE
SLESS
NA nyinginezo nyingi
Wasiliana nasi
0754763364
 
Naam
 
Winga wa kila kitu, umemaanisha nini mkuu?
 
Kila kijana dar anataka kuwa winga.
Kila mmoja anaweza kuwa na mtazamo wake ila ishu ya uwinga sijaona kama ina tatizo lolote ikiwa uaminifu utazingatiwa!

Kitendo cha kumsaidia mtu kupata bidhaa au huduma anayohitaji bila ya janja janja yoyote, Kwakuzingatia kanuni na sheria, naona hata kwa Muumba haina makosa!

Binafsi sijajua kwanini watu wana mtazamo hasi kwenye hilo!
 
Ni sawa hata mimi niliwai kuwa winga kwenye upande wa nguo na viatu, ila pia upande wa nyumba na viwanja kwa sasa nimeacha, lakini niseme tu.

Mawinga wengi wa bidhaa hawana future na ni kazi ngumu kuliko licha ya kuwa kuna uongo uongo wa kuwauzia watu vya juu bila mteja wala boss kushtuka hapo ndo huwa patamu (ile unamuuzia mteja kitu kichochoroni huku unampamba aamini ni Og kumbe famba ile ya mwisho) kiatu umemuuzia store ukiwa umemtoa dukani kwa boss kimya kimya, alafu unamset atulie mahali ukamletee na kiti unampa πŸ˜… store ni 7500....yeye analipia 30000 unamrudishia 1500 ya nauli alafu sasa 21000 unatia mfukoni πŸ˜…
 
Doh! hii ndo inapelekea winga wanaonekana matapeli!
Kwa style iyo hata mimi iyo kauli naunga mkono!
Siwezi support dhulma!
 
Hili linaweza kueleweka tofauti kutokana na utofauti wa kiimani ila sahau yote zingatia hili kwanzaπŸ‘‡

Ikiwa wewe ni Muislam!
Zingatia sana uhalali na uharamu katika utafutaji wako wa riziki!
Imekuwa ni kawaida sana kwa zama hizi kuangalia maslahi ya kidunia zaidi kuliko Akhera yetu!

Uongo, Utapeli, Riba na Kamari vimepamba moto.
Yote hayo ni kwasababu tumeyaweka mbele matamanio ya nafsi zetu kwa kuikumbatia dunia na kujisahaulisha kuhusu akhera!

KUHUSU WINGA NA UDALALI:
Kwa kweli haya mambo watu wanafanya tu ila yana taratibu zake kwa mujibu wa sheria ya kiislamu.

Sheria na taratibu hizo zinalengo la kutulinda sisi sisi, juu ya madhara ambayo hutokea pindipo watu wanapokwenda kinyume na sheria hizo!

Ilo lipo wazi, nadhani sisi wenyewe tunashuhudia matukio ya wizi, utapeli, ulaghai na kadhalika!
Yani imani imetoweka kabisa na maisha yamekuwa magumu mara dufu zaidi!
Yote hayo kwasabubu tumeyawacha mafundisho na kuzipuuza sheria na taratibu za dini ya Uislam.

Enyi Ndugu zangu katika Imani, tufahamu kwamba hayo yanahitaji mazingatio ya hali ya juu mno!

Kwa sasa sitoandika mengi sana, Ila huu ukumbusho naomba ukatufae sote, hata kwa wale wasio amini haki (Kafir) pia nao watafakari kwa kina, ili nao kwanza waje kwenye haki!
Halafu kwa pamoja tufuate muongozo sahihi!
InshaAllah Allah atufanyie Wepesi!


Naomba kwanza tusahau kuhusu hiyo post niliyopost kuhusu WINGA!
INSHAALLAH Nitaandaa post itakayoelezea namna sahihi ya kuwa Winga/Dalali mwenye mafanikio duniani na akhera, kwa kuzingatia sheria na taratibu za Uislam.
 
major kwenye products za kike mkuu utafurahi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…