Ninajiuliza na naomba kuelimishwa kwa kupewa faida na hasara. Kipi bora kwa mtoto aliyemaliza kidato cha nne. Kumpeleka kidato cha tano au kumpeleka Chuo kwa elimu ya juu.
Nawakilisha.
Nilichogundua elimu ya Advance ina zima ndoto za wengi, kuna wanafunzi walipenda kusomea udaktari leo hii wanasoma education, mtihani mmoja tu unazima ndoto ya mtu,
Mimi nilipomaliza form iv sikutaka kuendelea advance nilienda diploma direct na matokeo yangu yalikuwa mazuri tu sana, nilisoma miaka 3 nikamaliza nikaunga degree, leo nipo mwaka wa pili, Nilichokuja kubaini wale niliomaliza nao form iv karibu wote waliendelea na advance na ufaulu wao o-level ulikuwa mzuri tu sana,
Baada ya kumaliza form vi, wengine ndo wapo diploma mwaka wa pili sasa, wengine wanasoma Bachelor ila programmes ambazo hawakuwahi kuzifikiria na sio ndoto zao, na wengine walibahatika machaguo yao, Na mimi nilisoma kitu nilichokihitaji kupitia diploma. na mpaka sasa naendelea na Bch.
Tatizo elimu ya diploma imeshajengewa dhana na wanajamii kwamba ni sehemu ya failures ila si kweli, mzee wangu mwenyewe hakutaka kabisa kusikia kitu kinaitwa diploma, ila nilienda kibishi kwa msaada wa makaka.
Kwa hiyo ushauri wangu mpeleke diploma kama ameridhia, na akasome kitu anachopenda na anajua ata perform vizuri.