Kipi bora, kujiunga chuo au kidato cha tano?

Kipi bora, kujiunga chuo au kidato cha tano?

A lev ndo kabali yao kwakuwa huyo failure na ki3 chak cha mwsho kisishobalance aend zoom.
 
Ukimaliza diploma unaweza kwenda chuo na sehemu kubwa inakuwa ni marudio na profession unaielewa kwa undani zaidi.mimi nilipita A level ila wanangu sitawapitisha huko it is wastage.
 
Dah naona wengi mliochangia hii mada form six milangukia pua.
Komaa kijana nanda advance!

Mm nilipita A level wala ckuangukia pua ila kama yeye anajiamini na comb anayo taka kuchua basi aende A level ila kama alipita kwa bahat nasibu aende tu chuo
 
Ukilinganisha kwa mfano Dakitari, Engineer or mtalaamu yeyote ayelisoma degree baada kupata diploma ya miaka 3 anakuwa ni mzuri sana 10X kuliko huyo aliyepata Degree direct kutoka O-level, lkn kama anampango wa kusoma politics bora apitie advance lkn awe makini sana ubora wa shule atayokuwa anasoma advance.

Mimi nimesoma Diploma ya Technical na tayari Mwajiri wangu ambaye taasisi ya Serikali kashanipa kibali na ruhusa ya kusoma degree ya miaka 3 kuanzia mwezi wa kumi, wakati huohuo mshahara unasoma kila mwezi na kama bajeti ikiruhusu atanisomesha na siyo tena mkopo, nikashamaliza chuo mshahara huo niliokuwa nao unapanda.

Kwa hapo sasa yule shemeji aliyepita Advance hata kama amepata ufaulu mzuri wa A-level tayari nimeshamzidi kiuchumi miaka miwili na hata ngazi ya utumishi nimeshatangulia kwa mie tayari bosi wake. Hlf unawahi mapema sana kujitegea na kupunguza mzigo kwa wazazi, ndugu au shemeji zako
 
Ukimpeleka chuo atakwepa jeshi ila awe na uhakika wa kupata kaz yenye malipo kidogo au ya kusuasua kwa kuwa hatakuwa na cv sawa na yule alipita 4m 6.njia za mkato zina madhara mkuu
 
Advance maisha magumu.....npo MUST nasoma diploma ya civil engineering na asilimia kubwa tunaosoma nao wamemaliza advance na wanajuta kwenda huko.
 
Mimi nimepitia A LEVEL nimegundua ya kuwa hiyo ni kupoteza muda kabisa.
 
A-level si tatizo, tatizo ni kwamba utaenda a level shule ipi? km ni santi kayumba nenda tu chuo mi nlisom kibiti advance pcm, uchumi wngu/familia mbaya, hatukuwa na mwalimu wa hesabu mpaka tuko six ,

Umeme unawashwa saa 2-4 kamili usiku nikapaform kwa kiwango hafifu baada ya kustrago saaana...means si wote wana huo moyo but easly to give up bora chuo but be careful on advanced math soma tuit za kitaa kwanza.
 
Kama amefaulu vizuri hongera kwake,ushauri:akienda A level atasoma miaka miwili na kma atafaulu vizuri kuanzia div 1 hadi three ya kumi na sita basi ondoa shaka ataenda chuo na kusoma degree ila kwa course inategemeana na points kwenye masomo yake matatu ya Alevel

ila kama atafeli basi atakua amepoteza miaka miwili bure cha muhimu ni bora aende chuo direct diploma ya miaka mitatu na kuajiwa au kujiajiri direct maana hii kidogo ndio aitampotezea muda b'ze ameshapata taalumu yake directly........ni hayo tu mdau
 
Ukimpeleka chuo atakwepa jeshi ila awe na uhakika wa kupata kaz yenye malipo kidogo au ya kusuasua kwa kuwa hatakuwa na cv sawa na yule alipita 4m 6.njia za mkato zina madhara mkuu

Sio kweli labda unaongelea Bachelor VS Diploma.
 
Ninajiuliza na naomba kuelimishwa kwa kupewa faida na hasara. Kipi bora kwa mtoto aliyemaliza kidato cha nne. Kumpeleka kidato cha tano au kumpeleka Chuo kwa elimu ya juu.

Nawakilisha.

Nilichogundua elimu ya Advance ina zima ndoto za wengi, kuna wanafunzi walipenda kusomea udaktari leo hii wanasoma education, mtihani mmoja tu unazima ndoto ya mtu,

Mimi nilipomaliza form iv sikutaka kuendelea advance nilienda diploma direct na matokeo yangu yalikuwa mazuri tu sana, nilisoma miaka 3 nikamaliza nikaunga degree, leo nipo mwaka wa pili, Nilichokuja kubaini wale niliomaliza nao form iv karibu wote waliendelea na advance na ufaulu wao o-level ulikuwa mzuri tu sana,

Baada ya kumaliza form vi, wengine ndo wapo diploma mwaka wa pili sasa, wengine wanasoma Bachelor ila programmes ambazo hawakuwahi kuzifikiria na sio ndoto zao, na wengine walibahatika machaguo yao, Na mimi nilisoma kitu nilichokihitaji kupitia diploma. na mpaka sasa naendelea na Bch.

Tatizo elimu ya diploma imeshajengewa dhana na wanajamii kwamba ni sehemu ya failures ila si kweli, mzee wangu mwenyewe hakutaka kabisa kusikia kitu kinaitwa diploma, ila nilienda kibishi kwa msaada wa makaka.

Kwa hiyo ushauri wangu mpeleke diploma kama ameridhia, na akasome kitu anachopenda na anajua ata perform vizuri.
 
kama wewe ni mwelewa mpeleke f5,si tu kuangalia atavuna kipi bal elimu atayoipata n faida sana hata kwa maisha ya kawaida kwani atapanuka kiakili (reasoning,decision and understanding capacity)

Kama atasoma ART kuna uhakika wa kufaulu ila kama ni sayansi mwangalizie shule nzuri! SIKUSHAURI KABISA KUACHA F5 ILI AENDE CHUO.
 
Faida zipo kutokana na combi atakayo taka kusome maana siku hizi kama comb za science mfano PCB ukipata three tu mkopo utafanya kuusikia kwa wengine sasa hapo kama huna uwez uwiii udaktari ndio baibai

kama ni arts inategemea akipiga one au two ewaaa mkopo anapata ila kama mwenyewe hana n is na A level mpeleke tu diploma maana asje poteza muda bure na siku hizi utandawaz umeenea
Mkuu hapo si ungemwambia mapema aende chuo kuliko kuuzunguka mbuyu.......
 
Back
Top Bottom