Kipi Bora kukaa kwa kaka aliyeoa au Kukaa kwa dada aliyeolewa, wakati unajichanga maisha?

Kipi Bora kukaa kwa kaka aliyeoa au Kukaa kwa dada aliyeolewa, wakati unajichanga maisha?

Kimwakaleli

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2018
Posts
7,755
Reaction score
11,737
Habari za Leo Wanajf,

Katika pitapita yangu Leo jioni,Nimekuta mada ya watu wakibishana kuhusu swala la kukaa kwa hao ndugu!mmoja wa wachangiaji amedai anayekaa kwa dada anakuwa huru na Raha zaidi kuliko anayekaa kwa kaka aliyetoa!Hebu tupe maoni Yako mwanajf na sababu zako.

Ahsanteni.
 
Inabidi utafute sehemu yako ya kuishi ila kukiwa hakuna namna ni heri ukae kwa dada.

ukiishi kwa kaka yako kama bado hajaoa haina shida, Tatizo linapoanza ni pale akioa maana wanawake wengi wakiolewa huwa wanapenda nyumba iwe na ndugu zao tu, na hata kaka yako akioa atasaidia pia ndugu wa mke lakini mke wake atasaidia tu ndugu zake.

Hivyo ni heri uishi kwa kaka kama hajaoa ila akioa nenda kaishi kwa dada.
 
Kwenye maisha kuna wakati unalazimika kutoka kwenda mbali na familia yako (wazazi) ambako haufahamiki na wenyeji wa kule, ikitokea hivyo hasa kwa kuzingatia machaguo uliyoweka hapo juu ni bora iwe ni kwa kaka aliyeoa kuliko kwa dada aliyeolewa.

Kwenda kwa dada kwa lengo la kujitafuta kuna namna fulani heshima inapungua na hata wewe binafsi kama unajitambua kiume ni lazima utaishi kwa kujishtukia sana.

Italeta maana kukaa kwa dada kama umri wa kijana huyo ni mdogo na yuko pale kimasomo, sio mwanaume mzima na ndevu unakaa kula ugali wa shemeji.

NB: Unapokuwa kwa watu iwe kwa dada, kaka ama watu baki, msingi mkubwa ni kujituma kutekeleza kila unalohisi ni wajibu wako ili usionekane mzigo kwa mwengine.
 
Habari za Leo Wanajf katika pitapita yangu Leo jioni,Nimekuta mada ya watu wakibishana kuhusu swala la kukaa kwa hao ndugu!mmoja wa wachangiaji amedai anayekaa kwa dada anakuwa huru na Raha zaidi kuliko anayekaa kwa kaka aliyetoa!Hebu tupe maoni Yako mwanajf na sababu zako. Ahsanteni.
kaolewa dada ako siyo wewe. Huyo shemeji yako siyo ndugu yako.

Kakae kwa kaka yako umsaidie kazi za ziada usipende kufugwa kama kuku
 
Hizo sehemu zote mbili tazama kwanza usalama wa chakula Kama upo

Maana kwa nijuavyo wanawake kama chakula nitatizo utaishi kwa shida Sana .

Ukishaona usalama wa chakula upo angalia miondombinu kama nyumba n.k

Hivyo vyote vikowepo , itabaki tabia hakikisha unabadilika kuendana na mazingira.

Na mwisho kuwa MTU wa kujituma kufanya kazi hasa usafi wa nyumba ,vyombo nk

Kumbuka subra ndo ibada yenye malipo makubwa
 
Habari za Leo Wanajf katika pitapita yangu Leo jioni,Nimekuta mada ya watu wakibishana kuhusu swala la kukaa kwa hao ndugu!mmoja wa wachangiaji amedai anayekaa kwa dada anakuwa huru na Raha zaidi kuliko anayekaa kwa kaka aliyetoa!Hebu tupe maoni Yako mwanajf na sababu zako. Ahsanteni.
Kaa kwa kaka
 
kaolewa dada ako siyo wewe. Huyo shemeji yako siyo ndugu yako.

Kakae kwa kaka yako umsaidie kazi za ziada usipende kufugwa kama kuku
Ni kweli mkuu,ila kwa uzoefu wangu ni kwamba madada wanawapendelea ndugu zao kuliko wa kiumeni mkuu!
 
Habari za Leo Wanajf katika pitapita yangu Leo jioni,Nimekuta mada ya watu wakibishana kuhusu swala la kukaa kwa hao ndugu!mmoja wa wachangiaji amedai anayekaa kwa dada anakuwa huru na Raha zaidi kuliko anayekaa kwa kaka aliyetoa!Hebu tupe maoni Yako mwanajf na sababu zako. Ahsanteni.
Kama ni wakiume kaa kwa kaka alieoa ili umsaidie kumliwaza mkewe wakati kaka hayupo au akishindwa kutimiza majukumu yake.

Kama ni mwanamke kaa kwa dada alieolewa ili umsaidie shemeji yako wakati dada hajisikii vizuri.
 
Tafuta msikiti wa karibu na kwa dada, kulala na kufua masjid, kula kwa dada, utakuja kunishkuru!
 
Back
Top Bottom