Kipi Bora kukaa kwa kaka aliyeoa au Kukaa kwa dada aliyeolewa, wakati unajichanga maisha?

Kipi Bora kukaa kwa kaka aliyeoa au Kukaa kwa dada aliyeolewa, wakati unajichanga maisha?

Hakuna cha eti umekuta watu wakibishana,wewe sema tu kama unapima upepo hapa ili ujue unaenda kukaa kwa nani,

Kaa kwa wazazi wako au kaa Ghetto na masela mnachangishana mpaka utakapo kaa sawa.
Ni mawazo Yako mkuu,Nina kwangu na watoto nipo Kisasa _Dodoma nilijenga Zamani sana wakati huo mfuko wa cement Tshs 500.Acha dharau dogo .
 
Inabidi utafute sehemu yako ya kuishi ila kukiwa hakuna namna ni heri ukae kwa dada.

Wanaume wengi tukioa wala hatuna noma na ndugu wa mke lakini kwa upande wa wanawake wengi huwa wanapenda nyumba iwe na ndugu zao tu, kaka unaweza anaweza asiwe na tatizo ila mke wake anaweza kuleta matatizo.
Kabisa bora kwa dada angalau.
 
Habari za Leo Wanajf katika pitapita yangu Leo jioni,Nimekuta mada ya watu wakibishana kuhusu swala la kukaa kwa hao ndugu!mmoja wa wachangiaji amedai anayekaa kwa dada anakuwa huru na Raha zaidi kuliko anayekaa kwa kaka aliyetoa!Hebu tupe maoni Yako mwanajf na sababu zako. Ahsanteni.
Inategemea kama dada yako nae anachangia kwenye kipato cha familia big yes ila kukaa kwa shemeji dada yako anamtegemea mme wake na wewe mtu mzima unamtegemeabshemeji kidogo inakuwa na walakini.
Kwa kaka inategemea nature ya mke wake kuna wengine kuna wengine mpaka utaosha kila siku, sokoni na kufulia watoto wake usipo kaa sawa
NB inategemea watu hawafanani
 
Wote inategemea wako na tabia zipi.


Ila kukaaa kwa ndgu ni changamoto sana, fanya plan zako ukae muda mfupi.
Huenda wasikuchoke ila wewe mwenyewe ukajichoka.
 
Hapa lazima moshi utafukuta kabla moto hujalipuka!
Jifunzeni yalipozaliwa mahaba, Tanga:

 
Maisha haya!!kijana(shemeji wakiume) alikuja kwangu nikashangaa dada yake anapika vyakula aina mbili ,kumbe kijana anachagua vyakula tena akiwa kwangu,kitu ambacho ninaimani kama ndugu yangu wakiume asingethubutu.Nilipiga biti kwanza kwa Dada yake kisha kwa kijana.Walinielewa

Sent from my SM-A107M using JamiiForums mobile app
 
Kwa mtu mzima kukaa Kwa kaka au dada ni kujidhalilisha, kama hakuna namna, bora ukae Kwa kaka Yako maana huko ndo ufalme wenu uliko,,, kukaa Kwa dada aliyeolewa ni balaa zaidi maana huko ni ufalme mwingine
 
Wahi kwa dada haraka.... Ndugu wa mke mambo yao safi ila ndugu wa mume... Naishia hapo
 
Katafuteni Mashamba katavi mlime na kufuga//au kufanya shughuli nyingine,,hao ndugu zenu jitahidini wawawezeshe mitaji
 
Back
Top Bottom