Kipi bora kupekua simu ya mpenzi wako au kuipotezea

Kipi bora kupekua simu ya mpenzi wako au kuipotezea

tisa desemba

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2011
Posts
434
Reaction score
115
WADAU, naomba ushauri na mawazo yenu juu ya suala la kupekua (kukagua) simu ya mpenzi wako coz mwenzenu limezidi kuniumiza mara kwa mara!
Nikipekua cm yake sometime naumia mwenyewe, nikisema niipotezee cm yake naumia pia cz natamani kujua msg na calls zake........plz nishaurini.
 
pekua ila sio kiviiiiiiile hadi missed call jamaniyatakushinda
 
Pekua tu, ukimkamata ujue una Learner ndani, mfundishe jinsi ya kutumia simu effectively.
Na cheater, kuwa na simu mbili moja iache unakokujua strictly for business, nyingine inayojulikana mwachie mwenza wako aikagua hata akitaka na betri atoe aiangalie vizuri.

Na wewe mkaguzi, sasa unaumia nini, kumbe una engine ya korola afu unabeba body la samtrela, utapata kiharusi wakuzike bure afu huyo uliyekuwa unambania anakuja kulea wanao. Changanya za kwako...
 
unajua katika mapenzi lazima kuwe na openness so wewe pekuwa tuu kwani ni bora ujuwe unaibia mapema kuliko kuwa mjinga f
kwa muda mwingi....mapenzi yenyewe ya siku hizi usanii mtupu!!!!
 
Kama anatumia nokia na sms nenda kwenye SIM SMS utazikuta,kagua maana ukimwi noma
 
Sikushauri kukagua simu ya mwenzi wako kwa kigezo cha kutaka kujua mambo yake,kama atataka ujue mambo yake basi atakushirikisha katika kila jambo na akama hataki basi hata ukipekua hutokuta kitu na utabaki kuwa unahisi tu mambo yanavyokwenda na kuumia.
Kama kweli unampenda mwenzi wako,kwanini unaumia kwa kutojua anawasiliana na nani?Je yeye akifanya hivyo kwako utajisikiaje?
Unaonekana huna uhakika na mwenza wako na yafaa ujichunguze maana unaonekana unaishi kwa wasiwasi na huna amani na mahusiano.
 
Kinachokuuma sio simu ila mahusiano kati yenu.
HUMWAMINI mwenzako ndio maana una hitaji la kuchunguza simu yake.

Sasa badala ya kuchunguza simu jichunguze wewe mwenyewe.Jiulize kwanini humwamini alafu uanzie hapo.Kama kuna kitu aliwahi kufanya. . . ana tabia ya kukumbatia simu ama kunong'ona akipokea kaa nae chini umuulize kwanini hua anafanya hivyo.Wekaneni sawa kabla hujaambulia presha angali mapema.
 
Kama mwaminifu sim yake itakuwa hadharani lkn Kama sio ataifichaficha, kagua utoe hofu
 
simu lazima ikaguliwe...na kikiongezeka chochote kwenye simu yake/zake lazima ujue...
hii inajenga discpline kwa mwenzio!
 
Swali la kujiuliza:kwa nini unakagua...humwamini? na kama humwamini kwa nini uendelee kuishi nae...? utasema unampenda...ndo mapenzi gani hayo ya kutoaminiana!??
 
unajua katika mapenzi lazima kuwe na openness so wewe pekuwa tuu kwani ni bora ujuwe unaibia mapema kuliko kuwa mjinga f
kwa muda mwingi....mapenzi yenyewe ya siku hizi usanii mtupu!!!!
Hii ni surveillance, cm zangu haziguswi n vice versa, maisha matamu full kuaminiana
 
Swali la kujiuliza:kwa nini unakagua...humwamini? na kama humwamini kwa nini uendelee kuishi nae...? utasema unampenda...ndo mapenzi gani hayo ya kutoaminiana!??

Namwamini sana..........ila wasiwasi hauishi.
 
Discpline inajengwa kwa kukagua simu?
Yeah,,,,unamjengea mwenzi wako nidhamu ya uoga. Hawezi fanya mambo ya ajabu ajabu. Hata akifanya lazima ataplay smart.
Nafurahigi sana kuona my friends wanahakikisha wanadelete sms zote na kuclear calls zote kabla ya kwenda hom. Huoni hii ni discpline?
 
Hiyo ni discpline au ni unafiki?
Discpline ni kutofanya kitu unachojua hutakiwi kufanya na sio kukifanya kwa siri.
 
Back
Top Bottom