Kipi bora kuwa kiongozi wa kisiasa kama Waziri au Rais au kuwa mfanyabiashara mkubwa kama Mengi au Mo?

Kwa nini mkuu, toa sababu. Hutaki utukufu wa kulindwa na mitutu ya bunduki na kutembea kwa msafara wa ving'ora?
Yale machozi ya watu masikini na wanyonge wanaoonewa chini ya utawala wako sio mazuri,Bora maisha ya kuishi huru na kwenda kokote utakapo bila kuchungwa chungwa
 
Madaraka yanakuja na uwepo wa maadui wengi wenye uchu wa kukuua ama kukudhuru vibaya

Ila mtu Billionaire hao maadui wanatoka wapi ?

Madaraka hasa ukuu wa nchi ni ya competition ambapo anaeishia kupata ni mmoja, mara wengine waingie msituni kumwaga damu na mavita sababu ya kuingia Ikulu

Hiko kitu kwenye Mali hakipo

Na pia matajiri wanaishi maisha ya furaha ataenda popote bila ya ulinzi mkubwa akihofia labda majambazi na vibaka tuu, ila Urais mtu anakuwa anawindwa na maadui wa kila aina mara ukute kuna mataifa huko yanataka kumuua rais wa nchi fulani kwa sababu za kimaslahi,kisiasa,kimrengo na kadhalika

Kwa hiyo kimsingi Utajiri ni mzuri kuliko madaraka (hapa namaanisha Urais wa nchi/Ufalme wa nchi)
 
Trump ni bilionea, lakini mmm!
 
Utakuwa na hela sana mwisho utataka power tu, leo Trump anaweza kumuita Bill gate au Elon Musk muda wowote na jamaa akaenda ila ni ngumu kwa Bill Gate kumuona Trump muda wowote anaotaka.
Hayo mambo ya Afrika na nchi wasiojitambua. Trump hakuwa na uwezo wowote wa kumuita mtu kwa nguvu na huyo mtu atii. Tena kwa Marekani rais anapewa za uso hadharani, kwamba siendi au sitaki kukutana na rais na anapewa heshima ya uamuzi wake. Sio Huku kwetu rais anakuwa mungu mtu.
Mara ngapi wanamichezo wa Marekani wamekataa kwenda kuonana na Trump timu zao zinapochukua ubingwa?
 
Inategemea na mfumo wa utawala wa nchi uliyopo

Nchi zenye demokrasia na haki Money power is everything. Matajiri ndio wanaongoza nchi, ndio "wanachagua" viongozi wa nchi kupitia michango yao
Nchi za kwetu huku, political power is everything. Mwenye mamlaka ndio anayeongoza nchi, na ndio "anachagua" nani awe tajiri na nani awe maskini.

Case Study

Rugemalila na Harbinder ingekuwa Marekani wasingekuwa jela leo, huku na mabilioni yao wametulia Keko.
 
Wewe unapenda kipi
 
Money, Power (including political), very beautiful women and/or drinks. In that order.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…