Kipi cha kuanza pindi unapopata ajira: Kuoa, nyumba, biashara au gari?


Ukipata ajira cha kwanza ni kujifunza kwa nguvu zote kujua kazi mapema na kuimaster kwa uharaka.
 
Bado ni swali, nafikiri umeshajibu.
 
hivyo ni vipaumbele Binafsi na haviwezi kufanana kwa watu wote kwani familia zetu na mazingira yanatofautiana.
Kuna vitu vingi vya kuangalia hapo....mfano;
1. Umri wako
2. Kazi/kiasi cha mshahara unaopata
3. hali ya Familia yenu (kuna wanapata kazi wanategemewa, kulisha na kusomesha)
4. Eneo ulilopo (kuna eneo unahitaji pikipiki, ngombe wa kulima nk nk
5. kazi yako niya kudumu au ya muda (mkataba) nk
 
Katika makosa sikutaka kuyafanya ni katika KUJENGA.

Ukipata kazi alafu ukawa na akili ya kukimbilia NYUMBA basi hakika utajenga KIBANDA na si NYUMBA.

nyumba inategemea eneo, kwa haraka haraka hapa DSM eneo zuri kbs uwe na m10+ ya ARDHI pekee. hiyo hela kwa watu wengine tyr kashanunua kiwanja na kajenga KIBANDA (yeye anaita nyumba).

Kujenga NYUMBA ni mtihani sana sio jambo la kukurupuka tu.

Gari ni muhumu sana, na mm nilianza na GARI kwanza, nikaongeza ya pili huku nikiwekeza katika VIWANJA maeneo tofauti tofauti navipiga fensi natulia.

Baadae ndio nikaanza projects za ufugaji ktk kiwanja kimojawapo.

Then ikafata kujenga nyumba ya kwanza ikafata ya pili. Na cha kuchekesha siishi ktk hizo nyumba napanga. Maana nilihamishwa ktk Mkoa mwingine.

So in conclusion kujenga baada ya kupata kazi (immediately) si vizuri.. utajenga KIBANDA na si NYUMBA.
 
Uko sahihi sana mkuu. Binafsi Gari ni kitu cha kwanza,na ninanunua viwanja na kuviacha..
 
Tunafikiri sawa mkuu👍🏽 Mawazo yangu haya pia!
Nilipita humuhumu!
 
Kosa kubwa utakalo fanya ni kuoa aseeee usije ukaoa kabisa hapa Tanzania utajuta.
 
Inategemea na kipato chako, wengine tulianza kujenga na ni nyumba sio kijumba.
 
Hili jambo linauzito na linahitaji utulivu mkubwa wa akili pia maamuzi sahh,ila kwangu nafikir kujiwekez kwanz ili kupata/kujihakikishia kipato Cha kutosha hivyo vingine vinawezekan tu wakuu mathalani ukijijenga kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…