Kipi hupelekea Waislamu kutoa sadaka kiduchu licha ya ukwasi walionao?

Kipi hupelekea Waislamu kutoa sadaka kiduchu licha ya ukwasi walionao?

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
10,904
Reaction score
26,184
Ndugu zangu hapa nimekaa na masheikh wa msikiti wa hapa mtaani wanasema kuwa wao wangekuwa viongozi wa makanisa wangekuwa matajiri kwa kuwa Wakristo hutoa sadaka nyingi sio sarafu kama Waislamu.

Wamenihakikia kuwa kwa ijumaa ambayo ndio siku kubwa kwa wiki wao hupata elfu sita hadi kumi kwa msikiti wenye waamuni mia na zaidi kiasa ambacho ni pesa ya mtu mmoja kwa Wakristo?

Swali kwanini waislamu wanatoa sarafu huku pesa wanayo

USSR

USSR
 
Huenda
  1. Waumini wengi wanapokwenda msikitini hawachukui fedha....dhana ya ubahili siwezi kuisemea
  2. Hakuna maandalizi au tangazo rasmi la kukusanya sadaka, michango ya msikitini ni ya ghafla ukiondoa ijumaa kwa baadhi ya misikiti
  3. Mahitaji ya msikiti ni madogo, ni umeme, maji na hakiba kwa ajili ya dharura.... no hospital wala bendi ya muziki
  4. Hakuna imamu wa msikiti anayelipwa, wengi wao wanatafuta riziki kwa jasho lao
  5. Labda pawepo mfuko wa mayatima husika ndio patakuwa na uhitaji wa mamilioni ya shilingi ya sadaka
  6. Au pawepo shughuli ya ujenzi
 
Unapotoa sadaka hautoi sadaka ile kwa Padri,shekhe au mchungaji wako.Unatoa kwa sababu ya Mwenyezi Mungu sababu mwisho wa siku itasaidia kuboresha huduma ya msikiti, kanisa, hekalu.

Na pia itasaidia kukidhi haja za watumishi hao. Sadaka haijaanza leo sadaka ilianza tangu kipindi cha Abel na Kaini.Kuhusiana na wanaotumia hela hizi vibaya wachungaji, mapadri masheikh hukumu ni juu yake Mwenyezi Mungu kila mmoja atalipwa anavyostahili.
 
Waislamu hawana mambo mengi. Kanisani ukienda utakuta kuna mchango wa ujenzi wa nyumba ya mchungaji, vyombo vya kwaya, kanisa jipya, mkutano wa injili na mingine mingi. Mbali na hiyo michango kuna msisitizo mkubwa kulipa zaka 10% na sadaka 10% ya mapato yako. Yaani ukienda Church hadi urudi nyumbani tayari unakuwa na madeni kibao.
 
Sadaka si lazima iwe msikitini, sadaka ni jambo lolote utakalo lifanya na ndugu yako akapendezwa nalo. Basi hata kutabasamu mbele ya ndugu yako ni sadaka.

Lakini katika mafundisho ya dini kutoa sadaka nyumbani ndio Kuna malipo makubwa kuliko ile tunayotoa msikitini.

Nimeshawahi kumsikia sheikh Khamis Ame wa gongo la mboto anasema kuchangishana pesa msikitini kila baada ya swala ni bidaa (uzushi katika dini). Kama msikini unajiweza kujiendesha wenyewe hakuna haja ya kuchangishana pesa kila baada ya swala. unakuta msikiti una fremu za maduka na vyanzo vya pesa na unajiweza Kwa kila kitu hapo hakuna haja ya kuchangishana pesa.

Msikiti ni sehemu ya ibada tu, si sehemu ya kukamuana fedha, Fanya ibada zako, ukiona Kuna hitaji flani msikitini toa pesa yako au msaada wako, lakini kama kila kitu Kiko sawa basi kusiwe na utaratibu au mazoea ya kukusanya pesa kila baada ya swala kama wanavyofanya wakusanya Kodi.
 
Kuna msikiti magomeni walikua wanachangisha hela ya umeme,utasikia mwenye mia5,mwenye elf moja,aje atuchangie,nikasema duu sasa luku nayo mchango tena kwa miamia.

Ndugu wajukuu wa mudi,acheni ubahili na kutegemea waarabu kila kitu,soon mafuta yatakosa soko sijui mtapata wapi wafadhili.
Misikiti ipo Tanzania kabla hata mafuta hayajagundulika arabuni,Kuna siku waislam walikufuata kukuomba hela ya luku au maji!?
 
Kuna msikiti magomeni walikua wanachangisha hela ya umeme,utasikia mwenye mia5,mwenye elf moja,aje atuchangie,nikasema duu sasa luku nayo mchango tena kwa miamia.

Ndugu wajukuu wa mudi,acheni ubahili na kutegemea waarabu kila kitu,soon mafuta yatakosa soko sijui mtapata wapi wafadhili.
Me nafikiri approach nzuri ni misikiti kujiwekea mifumo mizuri ya kujiingia pesa zake yenyewe bila kutegemea sadaka.

Misikiti inaweza kuwa na miradi ya maduka, Kuna misikiti mingi imezungukwa na fremu za biashara. Hiki ni chanzo muhimu Kwa mapato ya msikiti. Pia misikiti ina na miradi kama shule, hospitali na vyanzo vingine vya pesa kuliko kutegemea waumini.
 
Swadaka na zakka't ndizo zinazotakiwa kuendesha misikiti,si kila msikiti una fursa ya kuweka frame za biashara au uwezo wa kuwa na shule au zaha ATI,waislam hawana kawaida ya kulipa zakka't,wameambiwa mpaka mtaji uzunguke mwaka bila kupata hasara ndiyo watoe zakka't
 
Back
Top Bottom