Ni mwaka ambao nimepita katika kila Aina ya vipindi.
Kiroho Ni mwaka nilioimarika Sana,MUNGU alinionyesha kipawa(karama yangu) na baada ya hapo nimepita sehemu ngumu Sana.
Ni mwaka niliopitia magumu mengi,Hadi kuna muda unafika nakata tamaa lakini bado MUNGU ananiambia nisimame.
Familia yangu imepita kwenye misukosuko Sana ila sikuchoka kuomba.
Ni mwaka ambao nimepata marafiki,
Wengine niliwaacha waende maana hawakujua umuhimu wa urafiki wangu na kujitoa kwangu,
Wengine bado nashirikiana nao katika kila Khali.
Hawa wote naomba baraka za Mungu ziwe juu yao.
Ni mwaka ambao rafiki yangu wa karibu(yumo humu) ameondokewa na Mama yake mzazi..hii Ni Jana tu.
Yote Yote kwa yote namshukuru Sana MUNGU.
Ametuagiza tushukuru kwa yote mema na mabaya.
Yeye Ni MUNGU na atabaki kuwa Mungu
Sent using
Jamii Forums mobile app