MSHINO
JF-Expert Member
- Jul 26, 2013
- 1,070
- 726
Wana jamii, kwa sasa tunashuhudia majimboni wagombea mbalimbali wakipambana kuwa wawakirishi wa wananchi. Ukizingatia wananchi wote hatuwezi kwenda bungeni kujadili maendeleo yetu. Hivyo ni lazima watu wachache wachaguliwe ili kuwawakilisha wananchi baada ya kufanya mikutano na wananchi hivyo kuchukua changamoto na mawazo yao.
Lakini baada ya uchaguzi kupita wabunge wengi huandaa sherehe kubwa tena nje ya majimbo yao kwa kufanikiwa kupata hiyo fursa. Binafsi sioni sababu ya mbunge kufanya sherehe kwa sababu anaenda kuwatumikia wananchi.
Wabunge wanafanya hivyo kwa kuwa hakuna taasisi au tume au idara ambayo inasimamia kazi za mbunge. Japo balaza la madiwani linatakiwa kuwasimamia wabunge lakini madiwani hawana nguvu hiyo kwa sababu hawana uwezo wa kuitisha uchaguzi mwingine iwapo mbunge anafanya yake badala ya kuwatumikia wananchi.
Kitu gani kifanyike ili mbunge aachishwe ubunge na wananchi iwapo atashindwa kuwatumikia?