Kipi kilikupelekea uwe mnazi kwa timu yako unayoishabikia sasa?

Kipi kilikupelekea uwe mnazi kwa timu yako unayoishabikia sasa?

INTROVERT MAN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2019
Posts
993
Reaction score
1,343
Mimi ni shabiki wa Man U kwa pale EPL na Spain ni Valencia CF.

Man U
Nilianza kuwa shabiki wake nikiwa shule ya msingi. Kuna rafiki yangu alikuwa kanunua gazeti jipya la michezo, basi katikati ya gazeti au page ya katikati mara nyingi huwa na picha za rangi na mara nyingi hubeba makala moja tu. Hiyo page ilikuwa imepambwa na picha kuuubwa ya Ruud Van Nistelrooy; picha hiyo ilikuwa imeenea pande zote mbili za katikati.

Nakumbuka hilo gazeti lilikuwa ni la mwezi May baada ya ligi kuisha na Man U ilikuwa imechukua ubingwa huku superstar wa msimu akawa Ruud Van Nistelrooy.

Kiufupi me ni msomaji mzuri wa magazeti tangu enzi hizo, basi ile habari ilinivutia kwa kweli nikaanza kuifuatilia taratibu historia na mafanikio mengine bila kusahau vipigo ilivyopata. Huo ndio ukawa mwanzo wa kuikubali Man U.

Valencia CF
Hapa bila ubishi nmekanyaga tabaka tawala. Kiufupi nilianza kuipenda mara baada ya kumiliki jezi yake ya msimu wa 1943|44 (hii mitumba bwana! joking)

Na hii timu nilizidi kuipenda mara baada ya kuona mabest zangu wamegawana timu 2 tu pale Spain: Barca na Real Madrid, basi mimi nikaona bora niwe unique kidogo.

NB: kwa hapa Bongo ni Yanga ambayo siyo siri marehemu mzee alinirithisha. [emoji5][emoji5][emoji28][emoji28]

Kwako wewe mdau, ilikuwajekuwaje mpaka ushabikie hiyo timu?
 
Mimi kwa hapa Bongo, Dar Young Africans. Hii ni asili - nyumbani sote Yanga. Kwa Ulaya ni Arsenal. Kisa cha kushabikia Arsenal nilikuwa nasoma madarasa sehemu moja inaitwa Kimamba maeneo ya Mwembechai kule, basi pale mwalimu wetu alikuwa bibi mmoja hivi na wanae kama watano (5) hivi, wote wa kike. Ile nyumba wote walikuwa Manchester miaka ile ya 98, 99 hadi 2005. Arsenal na Man U zilikuwa za moto vibaya mno; mara nyingi zilikuwa zinakutana kwenye makombe tofauti tofauti, kila nikiangalia wote wanashabikia Man U ile timu nyingine haina watu ikabidi mimi nijitenge kule, basi tangu hapo nikawa The Gunners - jezi zao mdhamini alikuwa "JVC", Man U mdhamini alikuwa "Sharp". Huku captain Vieira kule captain Keane; kila wakikutana lazima wazichape na kibaya zaidi walikuwa viungo, yaani ni lazima watakutana tu pale kati. Siyo hizi Man U na Arsenal za sasa hovyo kabsaaaaa!
 
Hata sijui kwa nini nlipenda The KOP mana mitaa hio ya 96 ilikua haifanyi vizuri, ila baadaye nkajua kua nlifanya maamuzi sahihi.
Forever Liverpool FC.

YNWA
 
Mimi kwa hp bongo Dar young Africans hii ni asili nyumbani soooote yanga kwa ulaya ni Arsenal kisa cha kushabikia Arsenal nilikuwa nasoma madrsa sehem moja inaitwa kimamba maeneo ya mwembechai kule basi pale mwalimu wetu alikuwa bibi mmoja hivi na wanae kama 5 hv wote wa kike ile nyumba wote walikuwa Manchester miaka ile ya 98 99 hadi 2005 Arsenal na Man u zilikuwa zamoto vibaya mno mara nyingi zilikuwa zinakutana kwenye makombe tofauti tofauti kila nikiangalia wote wanashabikia Man u ile timu nyengine haina watu ikabidi mm nijitenge kule basi tangu hapo nikawa the gunners jezi zao mdhamini alikuwa "JVC" Man u mdhamini alikuwa "Sharp" huku captain Vieira kule captain Keane kila wakikutana lazma wazichape na Kibaya zaidi walikuwa viungo yaani ni lazma watakutana tu pale kati sio hizi Man u na Arsenal za sasa hovyo kabsaaaaa!
Kama mimi aiseee......
 
Nakumbuka ilikua michuano ya kagame (Kagame Cup) sikumbuki mwaka kulikua na mechi kati ya Simba na Villa ya Uganda kipindi hicho bado dogo home wakiweka mpira hua nakasirika kweli nilikua napenda sana katuni.

Basi ile mechi Simba waliibuka na ushindi na nyumbani kaka yetu mkubwa ndiye aliyekua shabiki wa simba peke yake basi kwa kuwarusha roho mashabiki wa Yanga kaka alinunu kreti ya soda na kagawa kwa Kila mtu pale home na pesa juu.

Kwa kweli hii mbinu iliwateka wengi pale home basi toka siku hiyo nilitamani simba ishinde ili kaka atununulie soda na mwisho wa siku nimetokea kuwa shabiki mkubwa wa Simba.
 
Nakumbuka ilikua michuano ya kagame (KAGAME CUP) sikumbuki mwaka kulikua na mechi kati ya Simba na Villa ya Uganga kipindi hicho bado dogo home wakiweka mpira hua nakasirika kweli nilikua napenda sana katuni
Basi ile mechi Simba waliibuka na ushindi na nyumbani kaka yetu Mkubwa ndiye aliyekua shabiki wa simba peke yake basi kwa kuwarusha roho mashabiki wa Yanga kaka alinunu kreti ya soda na kagawa kwa Kila mtu pale home na pesa juu
Kwa kweli hii mbinu iliwateka wengi pale home basi toka siku hiyo nilitamani simba ishinde ili kaka atununulie soda na mwisho wa siku nimetokea kuwa shabiki mkubwa wa Simba

Mzee, bila ubishi huyo kaka yenu aliwapa rushwa takatifu tena wazi kabisa na kuwashika akili (joking).
 
2002 kombe la dunia Senegal alivyomwazilisha bingwa mtetezi nikavutiwa na hao wanyamwezi, sasa basi mtukutu El haji diof mpiga vyenga za mauzi nikapenda ujeuri wake wa kutemea mate mabeberu, mara pap Liverpool wakaomba huduma yake kule akakutana na wanyama akina Owen, Gerald, baros na wengineo basi tangu siku hiyo nikawa mnazi wa Liverpool
 
Upande wa bongo ni yanga, kuna mzee alikuwaga mnazi wa yanga miaka ya 96 so yanga ikishinda alikuwaga ananunua bunda la Jojo anatupa watoto wa pale mtaani tushangilie so nami nikawa mnazi wa yanga kupitia mazingira hayo
 
Mimi mwanzo nlikuwa napenda wachezaj tu na sio timu. Yan kila anaecheza akanifurahisha haijalish Tim gan mi napenda tu sijui pawasa, sekilojo chambua, kudra Omar, seleman matola, yan tafran. Niko form ll tumetoroka shule boarding kuangalia game ya simba vs yanga njia nzima kila mtu simba simba hapo nikajiunga rasmi na wananchi na kuwaacha wanafunzi. ## Yanga.

EPL bwana pia nkawa napenda soka LA mchezaj tu. Thierry Henry, Patrick Vieira nikawa the mshka bunduki ila sasa napenda pia soka la hawa waafrica soo an field pia Niko. Tim yyt kat ya hiz mi fresh tu.
 
Aisee miaka ya 2000 mwanzoni kuna couple ilipanga kwetu alafu walikua Simba damu, na kipindi iyo Simba kimataifani wapo vizuri mixer kuwatoa Zamaleck mara wakipige na Enyimba sasa hii couple ilikua inanichukua kwenda kucheki hizi games ndiyo hapo nikiwa Mnyama.
NB: Ilinichukua miaka kuja kujua kama kuna team ya chura, japo ni team ya baba na babu. International games zilinifanya niwe Simba.

Ulaya nilianza kuijua Real Madrid but mimi ni Gunner ile unbeaten na UEFA tunaingia final ndiyo nilikua naanza kupenda mpira.
 
Mimi ni shabiki wa man u kwa pale epl na spain ni Valencia cf.

Man u nilianza kuwa shabiki ake.nikiwa shule ya msingi kuna rafk angu alikuwa kanunua gazeti mpya la michezo.

Basi katikati ya gazeti au page ya katikati mara nyingi huwa na picha za rangi na mara nyingi hubeba makala moja tu.Basi hiyo page ilikuwa imepambwa na pocha kuuubwa ya Ruud Van Niestrooy .picha hyo ilikuwa imeenea pande zote mbili za katikati.

Nakumbuka hilo gazeti lilikuwa ni la mwezi may baada ya ligi kuisha na man u ilikuwa imechukua ubingwa huku superstar wa msimu akawa RVN.

Kiufupi me ni msomaj mzur wa magazeti tangu enzi hizo basi ile habari ilinivutia kwa kweli ..nikaanza kuifuatilia taratibu historia na mafanikio mengine bila kusahau vipigo ilivyopata. Huo ndio ukawa mwanzo wa kuikubali man u.



Valencia CF.
Hapa bila ubishi nmekanyaga tabaka tawala ..kiufupi nilianza kuipenda mara baada ya kumiliki jezi yake ya msimu wa 1943|44(hii mitumba bhna-joking)
Na hii timu nilizidi kuipenda mara baada ya kuona mabest zangu wamegawana timu 2 tu pale spain ;barca na real Madrid ,basi me nikaona bora niwe unique kidogo

N:B kwa hapa bongo ni Yanga ambayo sio siri marehemu mzee alinirithisha[emoji5][emoji5][emoji28][emoji28]

Kwako ww mdau ilikuwajekuwaje mpaka ushabikie hiyo timu??
liverpool for only the same name with king keagan during late 70's
 
Back
Top Bottom