INTROVERT MAN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2019
- 993
- 1,343
Mimi ni shabiki wa Man U kwa pale EPL na Spain ni Valencia CF.
Man U
Nilianza kuwa shabiki wake nikiwa shule ya msingi. Kuna rafiki yangu alikuwa kanunua gazeti jipya la michezo, basi katikati ya gazeti au page ya katikati mara nyingi huwa na picha za rangi na mara nyingi hubeba makala moja tu. Hiyo page ilikuwa imepambwa na picha kuuubwa ya Ruud Van Nistelrooy; picha hiyo ilikuwa imeenea pande zote mbili za katikati.
Nakumbuka hilo gazeti lilikuwa ni la mwezi May baada ya ligi kuisha na Man U ilikuwa imechukua ubingwa huku superstar wa msimu akawa Ruud Van Nistelrooy.
Kiufupi me ni msomaji mzuri wa magazeti tangu enzi hizo, basi ile habari ilinivutia kwa kweli nikaanza kuifuatilia taratibu historia na mafanikio mengine bila kusahau vipigo ilivyopata. Huo ndio ukawa mwanzo wa kuikubali Man U.
Valencia CF
Hapa bila ubishi nmekanyaga tabaka tawala. Kiufupi nilianza kuipenda mara baada ya kumiliki jezi yake ya msimu wa 1943|44 (hii mitumba bwana! joking)
Na hii timu nilizidi kuipenda mara baada ya kuona mabest zangu wamegawana timu 2 tu pale Spain: Barca na Real Madrid, basi mimi nikaona bora niwe unique kidogo.
NB: kwa hapa Bongo ni Yanga ambayo siyo siri marehemu mzee alinirithisha. [emoji5][emoji5][emoji28][emoji28]
Kwako wewe mdau, ilikuwajekuwaje mpaka ushabikie hiyo timu?