Kipi kimemfanya Geofrey Mwambe aliyekuwa Mkurugenzi (Director) wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kuteuliwa kuwa Waziri wa Biashara na Viwanda?

Alidhibiti vizuri uwekezaji kwa kuhakikisha wababaishaji na uwekezaji usiokua na tija kwa maendeleo haupati nafasi. Hao wababaishaji ndio wanaojidai wamekimbia.
 
Mkuu nimekuelewa sana ulichoandika japo wachache sana watakuelewa.
Kuna watumishi wengine wako very blind kutokana na ukosefu wa exposure hii inawafanya kukosa uweledi wa kufanya initiatives mbalimbali katika idara au wizara yake na matokeo yake anakuwa ni mtu wa kukaa tu ofisini kusubiria Boss wake atasema nini ndio afanye.
Ila on the other side utawala wa sasa ndio upo kwa staili hiyo yaani kwa mfano wewe umeteuliwa ukifanya kazi kwa kujiongeza mwenyewe na kuwa mstari wa mbele baadae unageukwa na kutumbulliwa mbele ya wananchi.
Utasikia anaanza kuongea mbele za wananchi"Mimi ni mtetezi wa wanyonge na huwa ninaumia kwelikweli wanyonge wakikandamizwa,nyinyi wananchi ndio mtasema nimfanye nini huyu jamaa.
Au ninasema uongo ndugu zangu?"[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Mwambe ni open minded Sana...

Pale TIC alibadilisha Sana ile hali ya "longolongo" iliyokuwepo miaka nenda rudi...

Watu aina yake ndio wanaofaa sana kuendana na KASI ya MAENDELEO ya VIWANDA....

Tunayategemea mazuri na MAKUBWA kutoka kwake.

Kila la heri kwake!!
 
U-TISS tu ndo unambeba

Duuu watu Mna chunguzaaa,
Watu mna deeo info!
Ila Hata kama ni TISS kuna Ubaya?
Hiyo sekta ni Muhimu sana ni bora achaguliwe TISS!
Ila Nimecheka sana sana Mkuu kama vile una Inside info???hahhaa
Ukitafakari sana....
 
Duuu watu Mna chunguzaaa,
Watu mna deeo info!
Ila Hata kama ni TISS kuna Ubaya?
Hiyo sekta ni Muhimu sana ni bora achaguliwe TISS!
Ila Nimecheka sana sana Mkuu kama vile una Inside info???hahhaa
Ukitafakari sana....
Habari ndo hiyo sasa; hint moja kuwajua hawa jamaa wanakuwa hawana Umahiri wala Ufanisi wowote kwenye nafasi wanazoshika lakini huwezi kuona waachwe kwenye nafasi za Utawala, sanasana wanakuwa wanahama tu mara hapa mara pale...

Na hata mwonekano wao, nguo wanazovaa nk. hawako presentable wanavaa kipolisipolisi tu, sura ngumu!

Mwambe alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni....mara vuuuuuumpuuu, Mkurugenzi wa TIC; na hapo hakuna alilofanya zaidi ya kuspy Wawekezaji au Wafanyabiashara wanapata wapi mitaji yao,halaf anareport kwa Jiwe,hakuwekwa pale kurahisisha Uwekezaji bali kukusanya taarifa za kiintelejensia za Wawekezaji

Kwa hiyo Mkuu.....akili za kuambiwa changanya na zako!
 

Sawa...
Ila inawezekana wengi wamechukia ulivyoandika[emoji851] au hawajakuelewa
Ila Nimekuelewa Mkuu!
 
chege mengi ya uliyoyaandika upo sahihi mno. Ila kwa wateule wa mheshimiwa wetu, Mwambe ndo reformer wa kweli kama ataachiwa afanye reforms na kama hatakuwa mwenye kuogopa unforeseen consequences za bwana yule. The guy is smart and ready to make changes. Shida iko kule tu njia ferry.
 
Akili mbovu za Kilumumba hizi manake huwa mnakurupuka tu na kuandika bila kuelewa!!

Hapa nimezungumzia suala la uwaziri au nimezungumzia Mwambe alivyokuwa TIC?!
 
Guys... simzungumzii Mwambe kama Waziri, nilikuwa nahoji exposure yake Mkurugenzi wa TIC. Nimeambiwa huko TIC alifeli, ndo nikahoji endapo alikuwa na exposure yoyote kwa sababu Mkurugenzi wa TIC anatarajiwa kuvutia FDI !!!

Ni kutokana na hilo, ndo maana nikamlinganisha na Julieth Kairuki... huyu hakuwa Waziri bali Mkurugenzi wa TIC!
 
Nakubaliana na wewe kwa 100% kwamba, pale inapobidi, unaweza kufanya hata head hunting kutoka nje ya mipaka!!!
 
Mkuu umeongea point tupu, japo simjui sana jamaa lakini nahisi ni mtu wa kitengo maana licha ya madudu kaula, amekuwa TIC kutokea kwenye uDC na pia ni memba wa bodies za BOT Na ttcl mobile.
Nimeona hiyo wakati najaribu kutafuta kabla ya u-DC kafanya kazi wapi na wapi!!!
 
Masisiemu Sasa ndio yamejua kiasi ambacho magufuli hawaamini.

Yaani kawapa Watoto wake, Na mbuzi za chadema alizonunua mnadani na zile ng'ombe za jalalani udsm pale bila kusahau lakezonelization, watu wa Kanda ya ziwa.

Masisiemu yamepigwa na butwaa
 
Ukiona mtu anakulaumu au kukuzodoa badala ya kukupongeza kwa unavyofananisha mchele na kunde basi jua huyo HAJUI AKILICCM ZILIVYO!!
 
BOT and Mimistry of Foreign Affairs & International Cooperation
Hayo pia nimeyaona lakini naona info kama bado chache mno! Kwa mfano hapo Foreign Affair, nimeona alikuwa Mkurugenzi wa Biashara BUT for ONLY one year... kabla ya hapo alikuwa anafanya nini... sijapata!!

Aidha, hapo BoT pamoja na TTCL nimeona akiwa tu Mjumbe wa Bodi!!! Matumaini yangu mtu kuwa Mjumbe wa Bodi, basi kawahi kufanya kazi hapa na pale... hicho ndicho sijaona kikijitosheleza; unless nami ni-conclude kama wengine kwamba inaweza jamaa ni Afisa Kipenyo!!

Lusungo
 
Ok, siwezi kuelezea exposure yake cause nna limited info juu ya kile nachofahamu kumhusu yeye, lakini katika hali ya kawaida kuwa mkurugenzi wa TIC kwa miaka hiyo mitatu, ni forum tosha ya kuwa na exposure na kutengeneza networks na Investors and Business Mogul. Ikiwa katika kipindi chake alivutia wawekezaji wengi kwa kiasi gani, hilo ni swali gumu lakini naamini hata ww una majibu yake. Muwekezaji kuwekeza Tz kwa sasa ni zaidi ya nani Bosi wa TIC. Hata Julieth angekuwa chini ya administration hii nadhani asingevutia hata unyayo wa muwekezaji. Backup ya top guy ni muhimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…