Je, jamaa ana exposure na dunia ya nje?!
Unajua kuna baadhi ya posts zinahitaji zaidi ya madgrii ya darasani na local experience bali exposure!!!
Hivi huyo Mwambwe anaweza kuinua simu na kumpigia Dangote na Dangote asiulie "Who? Mwambe??! Mwambe who? Come again?"
Anyway, nadhani nimeenda mbali sana!!! Hivi anaweza kuinua simu kumpigia hata Rostam Azizi?!
Ndo vile tu itakuwa ngumu lakini kama kuna Mtanzania anayeweza ku-fit hiyo position basi ni Mzee wa Msoga!!! Lakini ningekuwa JPM, hata watu kama Mwamvita Makamba wanaweza ku-fit compared na hao akina Mwambe!
Hawa watu wasio na exposure wanachoweza kufanya ni ku-attend Prospective Investors waliobisha hodi kwenye milango yao lakini sidhani kama wana ubavu wa kufanya "Investors Hunting" popote walipo duniani!!
JK pamoja na mapungufu yake mengi, alikuwa anafahamu sana nani akae wapi, na ndio maana akamvuta Julieth Kairuki ambae kabla ya uteuzi wake alikuwa kwenye banking sector huko South Africa na pia kuwa Project wa Private Public Partinership Capacity Building kwa nchi za SADC!
Kwa CV yake hiyo, tu tayari utaona Julieth kwenye mafaili yake alikuwa na orodha ya Wafanyabishara wa SADC ambao miongoni pengine alikuwa na uwezo wa kunyanyua simu na kuwapigia!
UPDATE:
Ukweli nilikuwa simfahamu kabisa huyo Mwambe lakini baada ya kuandika hayo hapo juu, nikalazimika kum-Google kidogo!!! Wallah JPM hayupo serious! Kumbe huyo jamaa kabla ya kuingia TIC alikuwa DC wa Manyoni?! Halafu ex-DC wa Manyoni ndie tulimpa dhamana ya kuvutia Foreign Direct Investment wakati hata akikutana na Diamond Platnumz tu lazima alikuwa anababaika!!!
Utani huu!!