Kipi kimemfanya Geofrey Mwambe aliyekuwa Mkurugenzi (Director) wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kuteuliwa kuwa Waziri wa Biashara na Viwanda?

Asante.. nitafuatilia takwimu kisha nitakurudia
 
Nice remark. ONYESHA. Usije na elimu ya makaratasi apa na maneno meeeeengi afu hatuoni output.

ONYESHA.

Ni vema tuambizane kipindi Mwambe ni MD wa TIC sisi kama Tanzania tuli-achieve nini kiuwekezaji ?
Rais wa Benki ya Dunia alikuwa na ni Daktari wa kutibu binanadamu.
 
Hapa kwetu unaangaliwa ukada tu
 
Hongera kwa Mchango bora kabisa. Naamini wengi tubadilika. Asante
 

Niliwahi kuandika humu zamani kidogo, tatizo la Tanzania tunatoa watu vijijini na kuwaleta mjini watuongoze.

Tunawaonea wivu waliozaliwa na kukulia mjini au hata wale waliokaa nje.

Tatizo lao kuu hawa waliotoka huko vijijini ni attitude yao. Baada ya muda mfupi sana wanajiona tayari wanajua kila kitu. Wanakuwa na kiburi na chuki dhidi ya wale waliowazidi maarifa. Hawataki tena kuwasikiliza wakidhani hiyo itawapunguzia heshima yao.
 
Mkuu: hii nayo utaiita exposure? Mtafute DC wa Kishapu, FDI yake ni 45%


Na hii nayo utaiita ni exposure? Hapa mtafute DC wa Mugumu two-thirds ya Serengeti iko huko, imo kwenye Alliance ya Kenya Airways gone awry. Ni hii:


Mtafute Waziri Mwambe umwangukie ukimtaka sahamani, Wafaransa wanakuja.

Umetaja mambo ya Lumumba, whatzzat? Mie ni mtu wa Vijijini, ila naujua ni mtaa maaroof Dar es Salaam, zamani ukiitwa Gloucester Avenue toka Pugu Road hadi Mtaa wa Narung'ombe kwenda Shimoni. Lakini hayo yanatuhusu nini?
 
Mwambe mwenyewe ameshindwa hata kujibrush ule mwonekano wake angalau umpe haiba ya Leader, mfano afuge hata mandevu tu, au aache nywele ndefu aka afro...always looks like mwanachuo tena mwaka wa kwanza first degree, uongozi ni haiba pia, ule mwonekano wa nje ndio unajenga kuaminiwa kabla hujasema neno, lakini wakati mwingine tatizo si Mwambe, tatizo ni waliomuona na kumpa hizo nafasi hao ndio tatizo pengine kuliko hata Mwambe, factor wanazotumia kumsaidia mteuzi ni dhaifu sana, kama ufaulu wa chuo ndio kigezo, kwenye zama hizi basi bado tuna safari ndefu sana kupata watu wenye uwezo kutatua changamoto tulizo nazo...ni ajabu Mwambe kupewa uwaziri wa viwanda tena ni first timer bungeni wanaachwa kina Bashe ambao tayari walikuwa wameonyesha uwezo kwny wizara walizokuwa...tuna kasoro kubwa sana kwenye vetting process iliyopo. Inawezekana tanzania tu, mtu anateuliwa siku ya siku anashindwa kusoma kiapo, kapitishwa pitishwa kote huko...mara Uded, mara kagombea ubunge mara ya kwanza kashindwa, mara ya pili kashindwa tena lakini akabebwa, unaona kabisa kuna watu wana bebana bebana tu, juzi naibu waziri wa teknolojia, Kundo wa hii wizara mpya, anahojiwa na media kitu gani kwny teknolojia anadhani kina mchango kwny maendeleo yetu...anasema inabidi tuwe na Instagram kwa lugha yetu, tusitegemee za wenzetu, fikiria huyo ndio waziri anasema hivyo, kwake kitu cha maendeleo kinachotrend akilini mwake ni kuwa na instagram zetu wenyewe hiyo ndio priority kichwani mwake, waziri wake Dr. Ndugulile baada ya kushindwa kwenye wizara ya afya wakati akiwa naibu tena kwenye fani yake, leo unampa wizara mpya ambayo hata si fani yake, unawaacha kina Profesa Mbarawa waliofanya vizuri term iliyopita angalau...ni mengi ya hovyo kabisa kuyasikia, sema tu sisi watz akili yetu ni nyepesi sana siku zote haitaki kuangalia mambo yanayofanyika kwa kina kujua kama yanatufaa au hayatufai...tatizo lipo kwa wanaomsaidia mteuzi, wao kwanza ndio walipaswa kushughulikiwa kabla ya kuwalaumu wanaoteuliwa!
 
Wakubwa salama!,

Naomba niseme machache.

Value ya TIC certificate ni ipi kwa sasa? Tic certificate value yake imebaki kwenye working permit class A tu na siyo tena kwenye uwekezaji (excemption).

Mwekezaji anakuja kuwekeza Tanzania anafika TIC, Tic wanampa check-list yao ambavyo akishakamilisha taratibu zote ikiwa ni pamoja na kulipa $1100 kama application fee.

Mwekezaji kapata TIC certificate of incentive anaorodhosheza vifaa vyake anavyohitaji kwa ajili kupewa msamaha wa kodi, TRA wanampa vifaa ambavyo ni 0 VAT vile vyenye VAT wanakata wanasema hivi haturuhusu. Sasa hapa tunavutia uwekezaji au tunafukuza wawekezaji.?


Kwa mantiki hiyo TIC Facilitation dept sioni haja ya kuwepo kwa sababu kampuni inaweza kupata excemption bila kupitia TIC na ndiyo maana TIC wanalalamika kukosa wateja siku hizi, value ya TIC certificate haipo tena.

Idara ya facilitation / Promotion imekuwa kituo cha polisi mwakilishi wa mwekezaji akifika anahojiwa nani kamtuma, analipwa kiasi gani? leta namba ya simu ya mhusika, namba ikitolewa anapigiwa simu mwekezaji na kuhojiwa maswali ya kiafande! Tunakaribisha wawekezaji au tunafukuza wawekezaji?

Facilitation hapo kuna miungu watu, mtu amechemka vetting mara ya kwanza why una unampa tena nafasi ile ile aliyechemka vetting?. Unatengeneza umungu mtu ndani ya huyo mtu kujiona kwamba yeye ndiye awezae tu.

Issue ya Ajira, kupata kazi TIC ni issue labda uingie kama secretary ukajiendeleze kielemu. Baada ya hapo ndiyo unakuwa ofisa. Na hao hao ndiyo wanakaa nakusoma Business plan za Wawekezaji, kazi ipo!

Shukrani!
 
Hizi ndo hoja sasa wakuu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…