Kipi kimezikumba hizi biashara za hawa macelebrity

Vhagar

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Posts
20,550
Reaction score
39,949
Dellaboss perfume ya Hajji manara hii aliizindua kwa mbwembwe zote huyu msemaji wetu wana msimbazi. Lakini sasa kimyaa hata mwaka haijamaliza.

Mofaya ya Alikiba, hii ni kama sijui kufata mkumbo maana tangu aizindue sikuwahi kukutana nayo kokote.([emoji3]sijui ndio kusema hapendi show off)

Chibu perfume ya Diamond. Hii nayo sioni chochote kikiendelea. Ila walio wahi kuitumia wanasema ni ya kawaida sana na bei ni kubwa mno(bei haiendani na bidhaa ni kama alikuwa anauzia jina)
Fynebyfalsafa ya Hamisi Mwijuma (mwana F.A), hii nayo naona kama haina maisha marefu maana hata promotion imepungua sana.

Mnaweza kuongezea biashara zingine za hawa ndugu zetu zilizokufa kifo cha mende.
Je, huwa wanakwama wapi labda?
 
Tatizo wana tegemea jina mtu kama Manara ana watukana wana Yanga juzi ana sema Zesco wasije na washangiliaji wao wapo utegemee mwana yanga anunue manukato yake hawajui biashara nini mdomo una weza kuathili biashara usipo uchunga..Pia biashara ina itaji mbinu na plan usitegemee jina
 
@kapeace,
Hata ile biashara kongwe kuliko zote umeshawahi kuifanya mtoto mzuri ?
 
Binafsi nimewahi onja mofaya kyela mbeya.. kwakweli zilikua nzuri... Cha kushangaa sehemu zingine kote sizioni..
 
Binafsi nimewahi onja mofaya kyela mbeya.. kwakweli zilikua nzuri... Cha kushangaa sehemu zingine kote sizioni..
Nilitamani siku moja niionje lakini sijabahatikaga kuipata.
 
hawapo serious na biashara....
unatangaza Tanzania nzima af unatuletea vi kontena 8 shenzi type

af hapo utakuta wako share hata 6 then wakipiga pesa wanagawana then mtu maarufu anasubiri aje mdau mwingine na wazo jipya maisha yaendelee
 
Mastar wabongo wanaofanya biashara kwa kujituma na mambo yanaenda

1. Esha salim buheti...huyu dada ni balaa kweye misosi

2. Shilole...nae ni mama ntilie biashara inakua

3. Jack wolper....house of bwangaz,huyu mchaga haa mchezo,

4.b dozen.....born2shine, huyu anajitahidi sana


Hizi ni biashara zakawaida zisizohitaji kiki na zinaenda fresh tu
 
hawapo serious na biashara....
unatangaza Tanzania nzima af unatuletea vi kontena 8 shenzi type

af hapo utakuta wako share hata 6 then wakipiga pesa wanagawana then mtu maarufu anasubiri aje mdau mwingine na wazo jipya maisha yaendelee
Lakini kitu kama kinalipa kweli mtu anashindwa vipi kukiendeleza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…