Kipi ndio bora Kati ya kuoa kwanza ndio utafute maisha ama uweke Mambo yako sawa kwanza ndo uoe?

Jipange kwanza kimaisha ndipo uoe, kinyume chake ni kukaribisha kudharauliwa na mke wako.

Vinginevyo kama bado mambo ya uchumi hayajakaa sawa, tafuta tu mchumba ila siyo mke.. utamwoa baada ya kufanikiwa naye
 
Nahisi ndo maana ndoa nyingi hazidumu ni kwa sababu ya mambo haya!

Wanawake wanaangalia biological clock kwamba, nikifika umri fulani naolewa, nikifika wakati fulani naolewa!

Wanaume nao wanaangalia financial clock kwamba, nikiwa na pesa kiasi fulani naoa. Nikinunua kitu fulani naoa!

hapa kati kati kabla hzo vitu vyao havijatimia hawawezi kuoa hata kama ni mtu sahihi.

Oa ukimpata mtu sahihi!
 
Nimekupata
 
Bora kutokuoa kabisa... Zalisha tu basi timiza kuhudumia watoto maisha yanaenda... 70% ya wanaume walio oa wamefeli kimaisha... 99% ya wanawake walio olewa wamefeli maisha...
 
Bora kutokuoa kabisa... Zalisha tu basi timiza kuhudumia watoto maisha yanaenda... 70% ya wanaume walio oa wamefeli kimaisha... 99% ya wanawake walio olewa wamefeli maisha...
Hizi takwimu ni za kimataifa, kitaifa, kimkoa, kiwilaya au umezipataje?
 
Aisee!🤔
 
Haujaona kilichomkuta bwana Emmanuel Jerome?! Alitaka kumuoa Bi Lucy Mshone ili waishi pamoja na kujenga maisha lakini balaa alilopitia limeishia na kifo.

Hiyo nguvu ya kupambana na ndoa ni bora kupambana na maisha utapata reward mwisho wa siku kuliko ukapambana na vituko vya mke au mwanamke ambaye hajaridhika na maisha ya kutafuta.
 
Hakuna formulae moja katika kutengeneza maisha yako mkuu. Kuna mtoto kapelekwa marekani baada ya muda amerudi na mke na watoto ila mwingine kaenda huko huko karudi shoga. Maisha ni kuchagua kile unachoamini ni sahihi kwako ili usije kuwa na majuto.
Mimi ukiniuliza nioe katika umri gani nitakakwambia at 30s sababu mimi ndio umri tayari starehe za ujana almost nimemaliza nimebakiza kwenda karaoke au kusafiri na mrembo wangu😊😊
 
ACha upuuzi wewe tafuta hela
 
Inategemea na mwanamke unaemuoa kama ni mvumilivu wa kuanza nae maisha,ana heshima,alafu kalelewa kwao maisha ya kienyeji 🤣.kama ana moyo huo wa kuvumilia na yeye anapambana,mambo yataenda.

Ila kama ndio hawa dada zetu wa siku hizi wanaoangalia kwanza income yako,gari unalo,utakuja kunyooka ,uchapiwe,akudharau 😆🤣

Bora uteseke ukiwa mwenyewe kwanza,kuliko kutaabika na mwanamke ndani.
 
Tafuta maisha
Kula bata
Jari afya
Ukiona nguvu zinaishia
OWA[emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…