Kipimo cha maendeleo ni kuwa na gari

Kipimo cha maendeleo ni kuwa na gari

kzba

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Posts
1,355
Reaction score
789
Asikudanganye mtu wala kukutia moyo, kama wewe huna gari hata kama ni mkweche unahesabika ni fukara tu hata kama una nyumba 50, tafuta gari upate amani ya moyo na heshima kwa wakwe hata kama huna hela.

Muhimu kujilinda, korona ipo na inaua fuateni miongozo ya wataalam wa afya jamani.

Kzba.
 
Kwa dar es salaam ,hii ni kweli kabisa juzi nilitaka vunjwa kiuno sim2000, wakati napita dirishani kupanda daladala za kuelekea mbagala rangi3, Ilibidi jamaa mmoja anunue maji ya 500 yenye barafu anichuwe mbavu.

Pale makumbusho ndio unaweza kaa hata masaa 4 usiku ukisubiria daladala za kuelekea maeno fulani, kamaa sii ufukara mtu unanunua hata kapasso kakupigia route ndogo ndogo. Imagine mtu unashikilia bomba la daladala kuanzia makumbusho hadi gongo la mboto sio mchezo.
 
Pole sana ndugu yangu pambana upate hata ka duet sio mbaya kinafika kwa wakwe hiko
 
Kwa dar es salaam ,hii ni kweli kabisa juzi nilitaka vunjwa kiuno sim2000 ,wakati napita dirishani kupanda daladala za kuelekea mbagala rangi3 , Ilibidi jamaa mmoja anunue maji ya 500 yenye barafu anichuwe mbavu,
Pale makumbusho ndio unaweza kaa hata masaa 4 usiku ukisubiria daladala za kuelekea maeno fulani, kamaa sii ufukara mtu unanunua hata kapasso kakupigia route ndogo ndogo. Imagine mtu unashikilia bomba la daladala kuanzia makumbusho hadi gongo la mboto sio mchezo
Ni kweli mkuu ,nyumba hazitembei.

Nilishangaa kuna jamaa ana maduka karibu 6 ya maana yenye worth karibu 180m lakin hana hata IST anapanda daladala bila barakoa! Kwasasa tusiwe na ile dhana ya zamani kwamba gari ni starehe,kuwa na gari ni sawa kuwa na simu etc
Huyo ni mpuuzi mwache afe na korona tutarithi hayo maduka
 
Wenye magari hapa tz wana stress sana! Yani mtu ana gari ila anaendesha kwa kujibana balaa, akifika tu kwenye foleni analizima eti mafuta.
Sawa lakini si ana gari somo ama! Inshu ni kuwa na gari haijalishi linatumia mkojo au matope
 
Kama huna kipato cha kueleweka na huna issue za maana zinazohitaji matumizi ya gari achana nalo..narudia tena achana nalo.

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Gairo
Mungu Ibariki Chakwale
Hizo ndio akili za mafukara, subiria sasa hiko kipato kikue ufe
 
Kama ilivyo kwa nchi yao kipimo cha kukua kwa democracy ni kutokuwa na upinzani!
 
Nyumba ni muhimu sana kama kijana wa kisasa kumiliki mjengo ni muhimu.
Nyumba inatembea ww? We tuulize sisi watembezi kama nyumba ina umuhimu, mimi nina nyumba mbili dar na dodoma, lakini sasa niko matimila huku songea hata sizitumii, ila niko na motokaa huku mwendo mdundo kitu cha toyota landcruiser Series 100, turbo peal white DUG 2006 nusu ya v8
 
Tatizo serekali yetu mpaka sasa kuagiza gari kwa mwananchi ni anasa maana kodi utakayo kutana nao utacheka.

Tokea 2000 gari duniani kote ni kama simu na lazima mwanadamu kuwa nalo.ila kwa tanzania serekeli bado ina husda
serekeli} = serikali
 
Tatizo serekali yetu mpaka sasa kuagiza gari kwa mwananchi ni anasa maana kodi utakayo kutana nao utacheka.

Tokea 2000 gari duniani kote ni kama simu na lazima mwanadamu kuwa nalo.ila kwa tanzania serekeli bado ina husda
Usiagize we chukua kwa wahindi wacheza kamali wa pale fire wanauza bei ya kutupa hata ukiwa 3milion unapata mkwaju kurudisha heshima kwa wakwe, yangu walinizia milion 43 na ni mpya kabisa
 
Tatizo serekali yetu mpaka sasa kuagiza gari kwa mwananchi ni anasa maana kodi utakayo kutana nao utacheka.

Tokea 2000 gari duniani kote ni kama simu na lazima mwanadamu kuwa nalo.ila kwa tanzania serekeli bado ina husda
serekali = serikali
 
Back
Top Bottom