Kipimo cha umasikini wa wafanyakazi wa serikali ni hiki hapa

Asili yetu ya kununua na kuuza Chakula siyo kwenye masuper market, na Wala siyo ndo utajiri...asili yetu na maisha yetu ni maduka makubwa ya nafaka, magulioni...na hata magengeni...uko ndo tunakoishi...hizo habari za supermarket ni za wazungu.
Mkuu sio asili yetu nikipato duni chetu mtu mwenye mshahaara wa 300k aende supermarket achague kipi ache kipi na hiyo 300k, ni bora kukimbilia kisando cha dagaa debe la mahindi na 5kg za maharage ili aendelee kuishi, hiyo siyo fashion ya maisha ni lazima.....otherwise utashindwa.
 
😆
 
Supemarket kufanya nini, punguza usasa.
 
Kwa hiyo ulitaka mshahara ukitoka wasiende kuchukua? Tuacheni na maisha yetu, wengi wenu mna njaa na mnatamani angalau mngekuwa waajiriwa.

My job, my salary.
Mshahara ukitoka familia Ile kuku, ivae, nipate bia kiasi na kulipa madeni fresh tu.

Kikubwa maisha yanasonga😂
 
Audacity ya kuwaita wengine umetoa wapi? Kuna mtu unamlisha hapa? Kapambania familia yako ,mengine ni kuleta umuhimu wako kwenye maisha ya wengine.
 
Hivi tajiri yukoje,zipi sifa zake?, Tuanzie hapo kwanza
 
Ulivyoandika robo kilomita nimekuona ni mwehu km wehu wengine
 
Asili yetu ya kununua na kuuza Chakula siyo kwenye masuper market, na Wala siyo ndo utajiri...asili yetu na maisha yetu ni maduka makubwa ya nafaka, magulioni...na hata magengeni...uko ndo tunakoishi...hizo habari za supermarket ni za wazungu.
Kweli mkuu huyu yeye anataka tufanane utamaduni na watu wa Ulaya wakati wenzetu wanatumia bidhaa za viwandani na sisi tunatumia bidhaa zinazotoka shambani moja kwa moja na kwenda kwa mlaji, mfano Nyama Ng'ombe ana chinjwa leo na analiwa leo na Maziwa yanakamuliwa leo kesho yana tumika na Kuku vile vile unaenda sokoni unachinjiwa unarudi nae Nyumbani, Sasa uko Ulaya Nyama na Samaki unakula wameshakaa zaidi ya miezi kwenye jokofu, na Juice na Maziwa yametengenezwa mwaka jana ndiyo yanatumika mwaka huu. Maharage na njegere zimeifadhiwa kwenye Makopo, na Wazungu wakija Tanzania wanaenda kununua Samaki na Nyama masokoni na siyo Supermarket.
 
Tanzania imejaa umasikini tu, iwe waajiriwa au waliojiajiri.

Bora hata waajiriwa wanajua tarehe fulani wanapata pesa, wengi wa waliojiajiri nanga inapaa. Fremu zimekuwa kama sare hapa mjini, kila mtu yakimshinda anakimbilia kwenye fremu.
 
Mkuu bidhaa za Supermarket ni tofauti na mitaani, Mtanzania siyo tamaduni yake kwenda Kununua mahitaji ya Nyumbani Supermarket ata hao Viongozi wakubwa wananunua mahitaji kwenye soko yetu, Kwa familia ya watu 6 ni ngumu kwenda kununua mchele kilo 50 na Unga wa ngano kilo 50 na Sukari kilo 50. Wanaenda kununua bidhaa Supermarket ni vitu vidogo vidogo kama Colgate, lotion, Maziwa ya Kopo na kahawa, Biscuit na Sabuni ndiyo bidhaa wanazoenda kuzinunua Watanzania na siyo bidhaa za vyakula.
 
Ninachoshangaa wengi wao wanaponda waajiriwa wengi n majobless wanatembea na bahasha kila sehem ila ss akikaa kwenye keybord ndo hao wanandika pumba izi
 
Yaani mtu kwenda kuchukua hela yake ambayo ni haki baada ya kufanya kazi kwa muda wa siku zaidi ya ishirini, unamuita masikini!?, kuitumia hiyo hela ambayo ni haki yake kununua vitu mbalimbali sokoni pia kwako ni umasikini? Kwako wewe ni nini maana ya umaskini? Au mshahara ni kwa ajili ya kazi gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…