Kipindi cha mwezi mmoja ni siku ngapi?

Girland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2016
Posts
2,489
Reaction score
4,253
Naamini JF ni home of great thinkers,unakopatikana uchambuzi na ufafanuzi wa hoja kwa kutumia mifano hivyo naona niilete hoja hii iweze kuchambuliwa.

Wote tunakubaliana ,kwamba kipindi cha miaka 1000 kinaitwa Millenium,miaka 100 Century, miaka 10 decade mwaka unaitwa year wenye miezi 12 ,sasa iweje miezi itofautiane idadi za siku? Yaani 28 au 29 au 30 na 31 na isifanane?

Hata tukiangalia vipindi vidogo navyo vinafanana mfano dakika zote zina seconds 60, siku zote masaa 24 wiki zote siku saba kwanini idadi ya siku katika miezi isiwe sawa? Kwa mantiki hio je ni sahihi kusema mwezi mmoja una siku ngapi ,karibuni
 
Zinatofautiana sababu za kiasili zaidi,kuna kipindi mwezi unatumia siku 28,30 na 31 kuzunguka dunia
 
Nashukuru mkuu, sababu nishawahi kumuuliza mtu, akabaki kunipa ngonjera tu.
 
Nashukuru mkuu, sababu nishawahi kumuuliza mtu, akabaki kunipa ngonjera tu.
Nawewe umeona eeh,maana haiwezekani basi wangetuambia siku zingine ziwe na masaa 25 zingine 26 na zingine 24 kama zote ni 24 inakuwaje siku za mwezi zitofautiane??
 
Mkuu mwezi una siku thelathini tu hayo mengine ya mapungufu au miezi mingine kuwa na siku nyingi zaidi ya thelathini ni ujanja tu wa watu fulani waliojaribu kubadilisha majira.
Kiufupi chunguza historia.
 
Mwezi una siku 27 au 28 ndio muda ambao mwezi huchukua kuzunguka dunia
Huo mwezi wa tarehe ulitengenezwa tu
 
A month is equivalent to 28 days.

Tukiwa chuo
Kila baada ya siku 48 tunatia timu kwa loan ofisa kidondosha saini.
 
Mkuu mwezi una siku thelathini tu hayo mengine ya mapungufu au miezi mingine kuwa na siku nyingi zaidi ya thelathini ni ujanja tu wa watu fulani waliojaribu kubadilisha majira.
Kiufupi chunguza historia.
Ndio maana mwezi ndio kipindi pekee ambacho hakilingani january si sawa na april wala february kwahiyo kuna ujanja mahali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…