niliona watoto wangu wanaangalia, kuna kipindi nikasema nikae nao niangalie nini wanakifurahia. mle ndani kuna maaudhui ya ngono sana na watu ndio wanapenda. maneno yanayochafua nafsi, watu wanatafuta kucheka/furaha toka kwa wanadamu, wanatafuta moyo wenye amani toka kwa wanadamu, wamesahau kwamba Yesu Kristo ndiye mfalme wa Amani na ni Mungu mwenye nguvu. amani yake atupayo sio kama ile ulimwengu utoavyo.
naasa tuwe makini sana na movie, tamthilia na series n.k, shetani ameingia sana. hasa wewe mtu wa Mungu, uwe makini kwasababu anachokifanya shetani ni kukurushia matone ya uchafu kidogokidogo baadaye utakuwa used to it na mlango wa yeye kuingia kwako utakuwa umefunguliwa, na hapo ndipo utakapopotea. wewe jiulize, hata ile wanaita JUAKALI ya dstv, na tamthilia nyingiii ambazo watu wanasema ni nzuri, KWANINI MLE NDANI LAZIMA AWEPO MWANAUME WALAU MMOJA ANAYE ACT KAMA SHOGA? wana mkataba gani na shetani? au freemason au chochote? kwanini tamthilia hata iwe vipi lazima mle ndani awepo mwanaume anayerembuarembua na kubehave kama mwanamke? why? na kwanini hizo ndizo zinazohit sana? zina upako toka wapi? upako huo ndio wewe ukiangalia sana unaambukizwa na baadaye unaenda kutenda dhambi kwa mlango ulioufungua wewe mwenyewe. Mungu awasaidie.