Kipindi hiki cha baridi nyanya ni upepo sokoni tenga lafika laki mbili

Kipindi hiki cha baridi nyanya ni upepo sokoni tenga lafika laki mbili

Papillon 1906

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
228
Reaction score
753
Kijana ukitaka kujiajili ingia kwenye kilimo cha bustani mazao kama nyanya,kabichi vitunguu nk. Hachana na kilimo cha mahindi ni umaskini mtupu lima mahindi ya chakula tu.

Nyanya inayopandwa mwezi wa pili mwishoni au mwezi wa tatu na kuanza kuvunwa mwezi wa sita mwishoni au wasaba ni muda mzuri wa kutengeneza faida tosha.

Kipindi cha baridi nyanya inachelewa kuiva na kupelekea kuwa adimu sokoni hivyo bei zake zinakuwa juu mara dufu.

Fikiria asa hivi sokoni nyanya tenga laki mbili pia kuna wateja toka mikoa kama masasi,mtwara na tunduru wanafika shambani moja kwa moja na kununua kapu moja mbaka elfu arobaini.

Kwa mtaji wa milioni moja na nusu unaweza kulima nusu heka na kupata mavuno wastani tenga 45-50 kama nyanya itakubali vizuri shambani.

Mtaji-1,500,000
Mavuno tenga 50
Bei sokoni 200,000

Kijana changamkia fursa,pia kama hauna mtaji wafanyakazi wanatakiwa wa kusimamia kwa miezi 4-5 ni laki 5 mbaka 6.

Toka magetoni
images.jpeg
 
Back
Top Bottom