Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
KIPINDI MAALUM CHA ALI MSHAM IBN TV AFRICA
Leo nimetembelewa na mtangazaji Hemed Lubumba wa IBN TV ili tufanye kipindi cha Ali Msham.
Ali Msham alikuwa mpigania uhuru.
Mengi tumeyapata kwa msaada wa picha zilizopigwa na mpiga picha maarufu wa nyakati zile za kupigania uhuru wa Tanganyika Bevin Tipha Msowoya.
Picha hizi ziko 11 ambazo marehemu Ali Msham aliwaachia wanawe.
Picha hizi zimetusaidia kueleza maisha ya Ali Msham na mchango wake katika kuitia nguvu TANU kupitia tawi lake la TANU alilofungua nyumbani kwake Mtaa wa Jaribu.
Historia yote ya Ali Msham In Shaa Allah mtaipata kipindi kitakapokwenda hewani.
PICHA: Picha ya kwanza kulia Ali Msham aliye katikati na vijana wa Bantu Group waliavaa kaniki na chini kulia ni Zubari Mtemvu, Julius Nyerere na John Rupia.
Picha ya pili ni Ali Msham ni huyo wa katikati akiwa katika mkutano wa ndani wa TANU nyumbani kwake Mtaa wa Jaribu.
Picha ya tatu ni wa kwanza ni Ali Msham akimkabidhi Mwalimu Nyerere samani kwa ajili ya ofisi yake jengo la TANU New Street.
Picha ya nne ni siku Tawi la Ali Msham Magomeni lilipofanya dua kwa ajili ya safari ya kwanza ya Julius Nyerere UNO 1955.