Tusalimiane Ivo Ivo tu hakuna namna.
Kila mwaka inapofika mwezi wa kumi balaa ndio huwa linaanza. Kama ni kipenga ndio kinapulizwa rasmi kuashiria kuwa goma ndio linaanza. Kama kujiandaa ndio kumefika Sasa.
Kipindi hiki huwa hakuna utulivu ni vurugu tupu kila kona, taa za mchina na vibatari zinatamakaki barabarani kwenye biashara na majumbani.
Ni kipindi cha mwezi wa kumi na kuendelea kila mwaka. Umeme unakosa kabisa utulivu, ukiathiriwa na upungufu wa maji kwenye mabwawa na miundo mbinu yake iliyo na changamoto nyingi za kiufundi na mipangilio ya umeme mitaani.
Hali husababisha maisha yanakuwa zig zag, yanakosa kabisa utaratibu.
Mimi utaratibu wangu wa kujiandaa ni huu. Nimenunua Vibatari koriboi tayari vipo ndani,mafuta ya taa ya kutosha tayari yapo ndani.
Siwezi kununua solar kwa kuwa solar inatakiwa ikae maporini kwa watema kuni na mkaa kusikokuwa na miundo mbinu ya umeme.
Mimi kwangu nimefungiwa umeme wa shirika langu pendwa natakiwa nipate umeme wa uhakika na sio umeme wa jua.Kuweka solar ni matumizi ya ovyo ya pesa wakati nyumba Ina umeme wa waya na nguzo.
Kazi kwako shuguli ndio inaanza na kipenga kinapulizwa.
Jioni njema.