Kipindi Tunamtafakari Dewji, Naomba atujibu Maswali Haya

Kipindi Tunamtafakari Dewji, Naomba atujibu Maswali Haya

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
17.03.2009.. Mo. Dewji aliinunua timu iliyopanda ligi kuu, ilikua ikiitwa Mbagala Market. Mda mfupi baada ya ununuzi huo, aliibadili jina na kuiita African Lyon.. Timu hii alidumu nayo kwa mda wa mwaka mmoja tu.. mambo yakawa magumu upande wake.. akaona isiwe tabu.. akaipiga bei kwa Ndg. Rahmu Kagenzi "Zamunda".

Miaka 5 baadae.. Mo. Dewji anaibuka na ndoto yake ile ile ya kutaka kumiliki timu inayoshiriki ligi kuu. Hapa anataka kujaribu bahati yake Simba S.C.. kwa kuomba apewe 51% ya umiliki wa Timu.. Huku yeye akiwekeza 20 bilioni katika Timu.

Simba S.C ni "taasisi" kubwa yenye fanbase kubwa pia.. Hivyo kuiongoza inahitaji uwe na "Moyo Mkubwa".. Je ule "Moyo Mdogo" uliokufanya ubwage manyanga African Lyon, sasa hivi umeshakua Mkubwa?

Je hivi sasa neno "hasara" halipo katika misamiati yako?.. Maana hofu yangu kuu ni kua mambo yakienda kombo katika timu yetu pendwa unaweza ukatutelekeza njiani.. huku ukielekeza lawama lukuki kwa wamiliki wengine [49%].. kua wanakwamisha mipango yako.

Kipindi Mo. Dewji anakabidhiwa Mbagala Market.. alikuja na ahadi hii.. ".. tayari nimeshanunua kiwanja ambacho nategemea kujenga kiwanja cha kisasa cha soka kitakachokuwa na viwanja vya michezo mingine kama vile sehemu ya gym, maduka na hosteli za kulala wachezaji"
Ndg. Mo Dewji miaka mitano baada ya ununuzi wa hicho kiwanja, maendeleo ya ujenzi yakoje?

USHAURI WANGU KWA Mo. Dewji.
1. Ndg. Mo. Dewji kama una nia ya dhati ya kuokoa soka letu, si lazima uje Simba S.C.. fuata nyayo za mabilionea wengine.. kwa kununua timu iliyo Ligi daraja la kwanza.. Hapo utakua huru kuimplement kila unachotaka kukifanya.
2. Kama ndoto yako ni kuifanya Simba S.C iwe ya Ki Ulaya Ulaya zaidi.. Si lazima uwe mmiliki.. Kuna bodi ya wadhamini, nadhani huko kuna "kiti" chako.

USHAURI WANGU KWA uongozi wa Simba S.C.
Kipindi tunaendelea kuipitia hiyo "paper" aliyoileta.
1. Naomba mkumbuke kumuuliza maswali hayo hapo juu.
2. Pia "Muwe makini.. Musije mkabidhi Mbu kazi ya kutibu Malaria"
 
Japo sipendi hizi team za mpira, lakini maswali yako ni valid...
 
Mikia acheni maswali mengi uzeni timu muache kukopa chapati kwa kaguduga, wewe uliyejipinda kuuliza maswali yote hayo unaweza kukuta sio mwanachama na hujawahi kuichangia timu ata elfu moja.
 
Poleni sana maana tonge lenu lipo hatarini kupokonywa ( watu wa getini,wauza jezi/bidhaa zisizoziingizia klabu mapato,na wacheza dili za ndani ya klabu) kwa sababu mwekezaji humu pote atapazibiti.
 
Mikia acheni maswali mengi uzeni timu muache kukopa chapati kwa kaguduga, wewe uliyejipinda kuuliza maswali yote hayo unaweza kukuta sio mwanachama na hujawahi kuichangia timu ata elfu moja.

Huo ulikua ni mtizamo wangu.. Na naheshimu maono yako.
Ila kwa taarifa tu.. Mi ni mwanachama wa Simba S.C.. na kadi yangu nimelipia hadi mwakani mwezi wa 9.
Nachangia vipi Timu yangu?
1. Kulipia kadi ya uanachama
2. Nimenunua jezi original za Simba toka katika duka la mtandao
3. Nimejiunga na Huduma za kupata habari toka mtandao wa Simu naotumia
4. Hua sikosi kuingia Taifa Stadium, Mnyama akiwa dimbani
5. n.k
 
Mo anataka dezo. Kabla ya Chealsea, Abramovic aliitaka Man U. Mambo yakagoma.
Bakheresa naye mnazi wa Simba alisoma alama za nyakati kaanzisha Azam yake.
Mo angekuwa kama Bakheresa leo African Lyon ingekuwa mbali sana.
Mo hana jipya.
 
Mo anataka dezo. Kabla ya Chealsea, Abramovic aliitaka Man U. Mambo yakagoma.
Bakheresa naye mnazi wa Simba alisoma alama za nyakati kaanzisha Azam yake.
Mo angekuwa kama Bakheresa leo African Lyon ingekuwa mbali sana.
Mo hana jipya.

Anaonekana anaiogopa sana hasara!
 
Huyu ni DEWJI aliyekuwa mbunge wa singida mjini?? Au yupi

Km ni huyo muulizeni ana viwanda vingapi kati ya dar na singida

Ana viwanda vingapi kati ya morogoro na singida

Ana viwanda vingapi kati ya singida na mwanza

Jibu ni kwamba amejenga viwanda sehemu ambako hakuwahi kuwa mbunge

Alisaidia timu gani ya singida angalau ikaingia hata nane bora kwenye harakati za kupanda daraja

Huyo mhindi aache utapeli..muhindi wa kuaminiwa Tanzania ni yule anayegombea ubunge pale Ilala peke yake hawa wengine ni ujinga mtupu
 
...wewe Sembo ni kweli mmefukuza kocha? na kama mmemfukuza kosa lake ni lipi?
#nimeona kwenye gazeti moja la michezo leo jmosi.
 
Angeniomba ushauri ningemshauri akainunue Mto ya Singida. Hivi Simba ni kampuni na inahisa?? Hisa moja inauzwa bei gani???
 
thamani ya simba ni kubwa kuliko bilioni 20 anazosema mo dewji, tatizo viongozi wa simba ama wapigaji au hawana fikra mpya bilioni 20 wanaweza kuzipata kama watauza jezi 2,000,000 kwa elfu 10 kitu ambacho kinawezekana ila utasikia jezi zitaingiza milioni 50 halafu wanachama wanashangilia.Anachotaka kufanya mo ni kufanya biashara kupitia washabiki wa simba ndio maana anaogopa kuwekeza kwenye timu nyingine
 
thamani ya simba ni kubwa kuliko bilioni 20 anazosema mo dewji, tatizo viongozi wa simba ama wapigaji au hawana fikra mpya bilioni 20 wanaweza kuzipata kama watauza jezi 2,000,000 kwa elfu kitu ambacho kinawezekana ila utasikia jezi zitaingiza milioni 50 halafu wanachama wanashangilia.Anachotaka kufanya mo ni kufanya biashara kupitia washabiki wa simba ndio maana anaogopa kuwekeza kwenye timu nyingine

Umenena vyema sana Mkuu.. Pokea like.
Moderator #BringBackVitufeVyaLike..
 
Last edited by a moderator:
Kasema simba hataki faida sababu ana biashara zaidi ya mia zinampa faida,yeye anataka timu ifanikiwe na mashabiki(akiwemo yeye) wapate raha.

Huyu jamaa ashawahi kuidhamini simba miaka ya 2000 nakumbuka na ilifanya vizuri sana kipindi kile.
 
Ha ha ha,hayo nayo unayaita mafanikio kulingana na umri wa simba?!!!!

Pia kwa taarifa, Simba S.C iliasisiwa mwaka 1936 [miaka 79 iliyopita].. Ikiwa na majina tofauti tofauti.

Lakini Simba S.C unayotaka kujua mafanikio yake ilikuja duniani mwaka 1971[miaka 41 tu iliyopita].. na mafanikio yake makubwa ikiwa kushiriki fainali ya kombe la shirikisho.
 
Back
Top Bottom