sembo
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 4,350
- 3,451
17.03.2009.. Mo. Dewji aliinunua timu iliyopanda ligi kuu, ilikua ikiitwa Mbagala Market. Mda mfupi baada ya ununuzi huo, aliibadili jina na kuiita African Lyon.. Timu hii alidumu nayo kwa mda wa mwaka mmoja tu.. mambo yakawa magumu upande wake.. akaona isiwe tabu.. akaipiga bei kwa Ndg. Rahmu Kagenzi "Zamunda".
Miaka 5 baadae.. Mo. Dewji anaibuka na ndoto yake ile ile ya kutaka kumiliki timu inayoshiriki ligi kuu. Hapa anataka kujaribu bahati yake Simba S.C.. kwa kuomba apewe 51% ya umiliki wa Timu.. Huku yeye akiwekeza 20 bilioni katika Timu.
Simba S.C ni "taasisi" kubwa yenye fanbase kubwa pia.. Hivyo kuiongoza inahitaji uwe na "Moyo Mkubwa".. Je ule "Moyo Mdogo" uliokufanya ubwage manyanga African Lyon, sasa hivi umeshakua Mkubwa?
Je hivi sasa neno "hasara" halipo katika misamiati yako?.. Maana hofu yangu kuu ni kua mambo yakienda kombo katika timu yetu pendwa unaweza ukatutelekeza njiani.. huku ukielekeza lawama lukuki kwa wamiliki wengine [49%].. kua wanakwamisha mipango yako.
Kipindi Mo. Dewji anakabidhiwa Mbagala Market.. alikuja na ahadi hii.. ".. tayari nimeshanunua kiwanja ambacho nategemea kujenga kiwanja cha kisasa cha soka kitakachokuwa na viwanja vya michezo mingine kama vile sehemu ya gym, maduka na hosteli za kulala wachezaji"
Ndg. Mo Dewji miaka mitano baada ya ununuzi wa hicho kiwanja, maendeleo ya ujenzi yakoje?
USHAURI WANGU KWA Mo. Dewji.
1. Ndg. Mo. Dewji kama una nia ya dhati ya kuokoa soka letu, si lazima uje Simba S.C.. fuata nyayo za mabilionea wengine.. kwa kununua timu iliyo Ligi daraja la kwanza.. Hapo utakua huru kuimplement kila unachotaka kukifanya.
2. Kama ndoto yako ni kuifanya Simba S.C iwe ya Ki Ulaya Ulaya zaidi.. Si lazima uwe mmiliki.. Kuna bodi ya wadhamini, nadhani huko kuna "kiti" chako.
USHAURI WANGU KWA uongozi wa Simba S.C.
Kipindi tunaendelea kuipitia hiyo "paper" aliyoileta.
1. Naomba mkumbuke kumuuliza maswali hayo hapo juu.
2. Pia "Muwe makini.. Musije mkabidhi Mbu kazi ya kutibu Malaria"