Kipindi Tunamtafakari Dewji, Naomba atujibu Maswali Haya

Kama moyo wake ni mdogo basi atachukua moyo wa tembo maana hakuna namna, maana nasikia moyo wa tembo ni mkubwa kama ndoo.
 
mi cjawahi kusikia mhindi anamiliki timu ya mpira wa miguu
 

Asante Mkuu.. Naamini wahusika wamekusikia.
 
Tatizo simba Ina wapenzi tu ila sio wanachama hai Kama kila mwaka hao unaosema wanachama 5mil wangekuwa wanapilia tu kadi zao za uwanachama kiasi cha elfu tano tu kwa mwaka embu Fikiri wangekuwa wanapata sh ngapi ila tatizo sisi porojo nja porojo

Nadhani hao wapenzi hawajaelimishwa vya kutosha juu ya umuhimu wa kuwa wanachama.. Wakati muafaka wa kuwaelimisha na kuwahamasisha zaidi wapenzi na wanachama umuhimu wa kuwa na kulipia kadi zao.. ni sasa.
Nasema ni wakati muafaka kwa sababu,
1. Timu inafanya vizuri katika ligi
2. Ile nguvu moja imerudi.. tofauti na msimu uliopita.
Ndg. Aveva.. mda ndiyo huu.
 
Wakati sisi tunajadili Mo kuwekeza sijui kununua % ngapi,TP Mazembe inazidi kuwaadabisha waarabu na kuleta sifa ukanda Wa chini ya jangwa LA sahara shangwe hiyo ikiambatana na kumpata kinara bora Wa ufungaji Wa mabao CAF champions league kijana Mbwana Samatta,nimesikia fahari kuangalia Aljazeera sports news wakitamka jina la kijana wetu Sammatta.
LA msingi Simba na Yanga wakilenga mikakati madhubuti inawezekana kufikia mafanikio ya TP Mazembe,wapiga deal wakiacha ufisadi.
 
Wapiga dili wa Msimbazi hawataki kabisa kusikia habari ya uwekezaji na umiliki wa timu kwa mtindi wa hisa...Bado miaka 50 mbele ndo Timu za Yanga na Simba zitazinduka....MPIRA PESA au hamuelewi maan ya msemo huu?..Leo TP Mazembe inafanikiwa kwa sababu ya umiliki wa mtu binafsi kama Moise Katumbi....
 
Kasema simba hataki faida sababu ana biashara zaidi ya mia zinampa faida,yeye anataka timu ifanikiwe na mashabiki(akiwemo yeye) wapate raha.

Huyu jamaa ashawahi kuidhamini simba miaka ya 2000 nakumbuka na ilifanya vizuri sana kipindi kile.
Kasema? Na wewe ukamuamini...

Anachotaka kuifanyia Simba kwanini hakuifanyia Mbagala Market? Simba iliwahi kufanya vizuri, ila aliyenufaika zaidi ni MO kutokana na kutangaziwa bure bidhaa zake za Safi, MeTL achilia mbali dili za kijanja alizodaiwa kufanya akiwa na simba.
 

Mkuu hebu punguza hizi porojo zako sidhani kama wanachama wa Simba wanafika hata 100,000 na hapa bongo hao mashabiki wengi wananunua hizo jezi feki.Kuna haja ya kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa hizi klabu otherwise usitegemee maendeleo yeyote
 
Haya mambo yalianza mwaka jana
 
Mkuu hebu punguza hizi porojo zako sidhani kama wanachama wa Simba wanafika hata 100,000 na hapa bongo hao mashabiki wengi wananunua hizo jezi feki.Kuna haja ya kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa hizi klabu otherwise usitegemee maendeleo yeyote
Mkuu tatizo la Watanzania hatupo business minded. Bado tupo katika zama za ujima kutegemea misaada, wafadhili, donations I mean term yoyote ile utakayotumia. Mwaka 1994 Mengi aliposhauri Yanga iendeshwe kibiashara wajinga wajinga walimjia juu hawakumwelewa na nina uhakika hawaelewi alichosema hadi sasa. Tunaogopa mabadiliko tunadhani timu ikiendeshwa kibiashara, ikununuliwa eg Dewji anavyotaka ni kwamba haitakuwa Simba tena , vizee visivyoweza hata kununua karanga havitakuwa na cha kuongea, kujivunia, yaani akili zetu zipo porini porini. Tunashindwa kuangalia na kuelewa kwa nini vilabu vikubwa afrika(TP Mazembe, Kaizer Chiefs etc) South America, na ulaya vinavyojiendesha na bado vina wapenzi sugu kuliko hata sisi ushuzi maharage. Nakumbuka hayati Mziray alisema pindi Simba na Yanga zikifa basi kuna watu wengi Dar es salaam pia watakufa kama nzi, sasa nakubali na hili. Mwanzilishi wa mada hii ambaye ni mpenzi wa Simba anathibitisha msemo huo wa hayati Mziray. Bottom line Mfumo wa uendeshwaji ndio kikwazo kikubwa kwa mafanikio ya vilabu vyetu.
 
Simba msimuuzie huyo Mo timu yenu mtaja chekea choloni, shauri yenu!
 
Acheni wivu wa kike team mmeshindwa kuiendesha kwa kukosa akili acheni watu wenye akili wawekeze
 
Hamna haja ya kuenda mbali kuangalia mfano wa TP Mazembe. Azam ni mfano tosha. Akiwekeza hizo billion 20 hata kwa Lipuli, itafika mbali
 
Nyie ndo mlikua mnategemea kusomesha watoto zenu na kununua magari na ela za club sasa mnaona mtakufa njaa mor akichukua timu ona leo mmeumbuka Aveva anahamisha ela ya club kwenye account yake binafsi hata aibu hamuoni shame on you
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…