Kipindi unajitafuta, michongo gani ulikua unapiga ili kujikimu kimaisha?

Kipindi unajitafuta, michongo gani ulikua unapiga ili kujikimu kimaisha?

Wote tunapitia vipindi tofauti mpaka tunakaa sawa,Kuna vipindi life linakua tight sana yaani ukija mchongo wowote huachi.

Michongo niliyoifanya kipindi nipo mavumbini ni
-Kuuza bando mtandaoni
-Kuuza links za utamu(hii ndio ilininunulia vitu vya geto )
-uwinga (hii ilinifungulia milango mingi sana)


Wewe michongo gani umepiga kipindi unajitafuta?
hustling isn't hobby
Ubungo bus terminal -nmekatisha ticket sana
South Africa /Nairobi

nipo bongo sijajipata Bado lakini Bora Leo kuliko jana
 
Nimemaliza bachelor degree ya economic and finance chuo cha uhasibu arusha wakati kikwete ndio anamalizia malizia muda wake, nikaingia mtaani. Safari ilikua na miba na mabonde ingawa sijapitia ugumu mkubwa sana.

1. Kubet. Mchongo wa kwanza ulionipokea mtaani. Hii naifanya mpaka leo lakini nimeboresha zaidi, saiv stake kidogo pesa nyingi. Wikiend nikiingia bar watu wanajiuliza jamaa anatoa wapi hela. Uzuri mimi sio mchoyo wa code za kupiga hela, wanaonifata kuniuliza huwa nawaonyesha tu mikeka. Odds 3 stake milioni 1, wanaogopa kuweka mzigo.

2. Msaidizi wa muuza chipsi. Nilitaka kuanzisha biashara ya chipsi lakini sina abc zake nikajisogeza kwa mwana kuomba nimsaidie lakini mpango wangu wa siri ulikua nikae pale kwa mwezi mmoja tu kujifunza biashara inaendaje.

3. Kibanda cha chipsi. Baada ya kupata ujuzi nilipewa mtaji na ndugu yangu nikafungua biashara ya chipsi baada ya miezi michache kadhaa nilipata kazi benki moja hivi kubwa hapa bongo. Kibanda cha chipsi nikamweka kijana. Kutokana na kutokua na muda wa kufatilia kwa karibu na changamoto ya uaminifu biashara ya chipsi ikafa.

4. Wakati wa magufuli benki ziliyumba ambao tulikua ranks za chini tukapunguzwa kazini. Nikarudi tena mtaani kudadadeki.

5. Lecture wa mchongo wa hesabu, uchumi na finance . Mtaa mgumu balaa, sasa geto kwangu ni karibu na chuo cha uasibu pale kurasini kwa sababu nilikua nafahamiana na wanafunzi pale na wengi walikua wananifata niwaelekeze maswali ya hesabu, graphs za economics na mambo ya finance. Nikaona kwanini nisiwe nawapigia pimbi kwa malipo? Nikawa lecture wa mchongo. Nawaelekeza mambo magumu ya darasani halafu wananilipa.

6. Finance and accounting officer usaid. Katika interactions za hapa na pale nilikutana na mshkaji wangu mmoja hivi nimesoma nae azania secondary kwa sasa jamaa ni diaspora uko marekani. Kitaaluma ni daktari. Akaniunganisha kwenye network yake nikapata mchongo usaid, kwenye kitengo cha masuala ya fedha. Wazungu Mungu awabariki sana, jamaa wanalipa vizuri sana. Nimefanya nao kazi takribani miaka minne.

7. Sasa hivi nina kikampuni changu binafsi. Bado sijafika ninapojiona lakini gari na nyumba sio ndoto yangu tena. Nipo kwenye hatua ya kuwaza legacy nitakayoiacha kwenye familia au jamii yangu.
 
Back
Top Bottom