Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Bado tunazungumzia nadharia ya kila kitu kuwa na chanzo ambapo wewe bado hujakubaliana na hiyo nadhari.
Mimi nimesema sijui

Wewe unayejua hujanijibu chanzo cha mungu ni nini?
 
Kwasababu mnapenda kusema mungu yupo bila uthibitisho, na kuombwa uthibitisho ndio udhaifu wenu
Suala la uwepo wa Mungu linajulikana ni imani hivyo si shida sie kusema Mungu yupo, kwahiyo kuombwa uthibitisho sio udhaifu kwetu bali ni udhaifu kwenu.
 
Suala la uwepo wa Mungu linajulikana ni imani hivyo si shida sie kusema Mungu yupo, kwahiyo kuombwa uthibitisho sio udhaifu kwetu bali ni udhaifu kwenu.
Nyie kwenu inawezekana sio shida kwasababu hamjaweka kipaumbele katika kujua ukweli, ila mimi nahoji kujua kama ni kweli

Kwasababu muongo yeyote anaweza kutumia trick kama hiyo kupenyeza uwongo wake, so utakubali kua uwomgo huo ni kweli kwasababu ni mambo ya kiimani?

Au utakubali kua madai hayo ni ya kweli kwasababu kuomba kwako uthibitisho wa ku verify hiyo habari kutakufanya uonekane dhaifu?
 
Mara nyingi nimekuwa nikiwaza huyu member hapa JF atakuwa alikutana na incident iliyomfanya akamchukia Mungu.

Hapa anaeleza namna alivyokuwa anasali na Nyerere pale St Peters




My take, huyu anahitaji kuombewa ili amrudie muumba wake.
Mshana Jr
Kusali SI HOJA mbona huko kwenye kusali wapo WACHAWI wengi tu!? Hoja ni kujua unasali na unamuabudu NANI!? Hiyo ndiyo hoja!
 
Hapo ni wewe ulisema haiingii akilini kusema kitu hakina chanzo, chanzo cha mungu ni kipi?
Kwahiyo kusema kuwa kila kitu lazima kiwe na chanzo ndio maana yake lazima nijue kila chanzo cha kila kitu?
 
Kwahiyo kusema kuwa kila kitu lazima kiwe na chanzo ndio maana yake lazima nijue kila chanzo cha kila kitu?
utajuaje kua kila kitu kina chanzo kama hujui vyanzo vyake?
 
Nikikwambia mimi ndiye Mungu mwenyewe, una uwezo wa kuthibitisha au kutothibitisha hilo?
 
utajuaje kua kila kitu kina chanzo kama hujui vyanzo vyake?
Iko hivi, sio lazima nimjue ni nani aliyevunja kufuli ya gate langu na kufungua gate ndio et niweze kusema kuwa kufuli ya gate langu imevunjwa na mtu na si kwamba imevunjika yenyewe na gate likajifungua lenyewe. Kwa kutumia akili huwezi kufikiri kuna uwezekano wa kufuli kuvunjika iyenywe na gate kujifungua lenyewe haingii akilini.

Kwahiyo ni sawa vitu kuwa havina chanzo ni jambo ambalo haliingii akili na haihitaji nijue chanzo cha kila kitu.
 
Kwenye mabishano ya vijiwe vya kahawa ulichokiandika kinaweza kua hoja ila sio hapa, mfano wako ni irrelevant kwasababu watu wapo na wanathibitishika kua wapo ni tofauti sana na mtu anayesema jambo fulani limefanywa na mungu ambaye hathibitishiki kua yupo na ukaweka assertion kua yeye ndio kasababisha

Ni sawa na mimi nikuambie kufuli lako halijavunjwa na mtu limejivunja lenyewe na wala sihitaji kukuthibitishia kua ni kweli kitu hicho kinaweza kutokea kwasababu hata kama siwezi kukuthibitishia kua kufuli halijajivunja, haitathibitisha kua kufuli halijajivunja. Umeona?

Kwa hiyo kama sio lazima kujua ukweli kwa uthibitisho, maana yake sio lazima kuwa sahihi kwenye hayo madai yako ambayo hayajapitia uthibitisho
 
unauliza maswali ambayo nisha elezea mapema kabisa

Nilivyokuambia kua kila kilichomo ndani ya ulimwengu kimesababishwa na ulimwengu except ulimwengu, ulielewaje?
Ulimwengu unawezaje kusababisha kila kilichopo? Thibitisha kisayansi na sio kinadharia wala kufikirika. Ukisema tu ulimwengu umesababisha kila kilichopo huo ni muujiza na si sayansi. Yaan ulimwengu umesababisha kila kitu kimiujiza sasa wewe utakua Atheist kweli? Au unaamini miujiza ya ulimwengu?

Thibitisha kisayansi ulimwengu umeform vipi vitu vyote hivi? Na si nadharia ya kufikirika unayoniambia hapa.
 
Kwenye kukubali kuamini jambo huwa hatutumii uthibitisho bali hutumia sababu na dalili za kuamini hivyo, kama ukiwa na uthibitisho wa hilo jambo sidhani tena kama utasema unaamini hilo jambo.

Je, tupo pamoja hapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…