Mabaya ni yapi? Unajuaje hili ni baya na hili ni zuri?
Nimeomba unipe metrics zitakazotumika kupima usahihi wa namna ya kuthibitisha uwepo wa Mungu na haujajibu.
Mimi hata siendi kwa vipimo vyangu.
Mimi nafanya "immanent critique".
Tuseme nakubaliana na wewe Mungu yupo (for the sake of argument, tupate sehemu ya kuanzia).
Na katika kukubaliana nawe hivyo, nakubaliana kwamba mambo ambayo kwa mujibu wa maelezo yako ya uwepo wa Mungu yamesemwa, ni kweli.
Kwa mfano, dhambi zipo na ni mbaya, kuua, kuiba, majanga, ni mambo mabaya.
Sasa nakuuliza, ili nipate kumuelewa vizuri huyu Mungu.
Mmesema huyu Mungu ana uwezo wote, ujuzi wote, upendo wote.
Kwa nini hakuumba ulimwengu huu uwe ambao mabaya hayawezekani, watu waishi na mazuri tu?
Ukijibu kuna ulimwengu huo mbinguni, hilo si jibu, mimi siulizi kama kuna ulimwengu usioruhusu mabaya, nauliza kwa nini hakuumba huu usiruhusu mabaya.
Mungu ambaye anaruhusu mabaya yasiyo idadi yaendelee miaka nenda rudi kwa kisingizio kwamba kuna ulimwengu unaokuja hautaruhusu mabaya atakuwa mkatili sana.
Ukisema katupa uchaguzi wa mabaya na mazuri, hilo si jibu, sijakataa kwamba katupa uchaguzi wa mabaya na mazuri, nauliza kwa nini kaachia mabaya yawezekane wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?