Sijakataa kwamba huo ni uhuru wake.Huo ni uhuru wake kuamua ulimwengu uweje.
Nimeshakujibu hili swali lako kwamba tayari ameuumba ulimwengu ujao usiokuwa na mabaya. Uwezo anao na ndio ameamua hivyo kwenye mali yake. Hakuna wa kumpangia.Sijakataa kwamba huo ni uhuru wake.
Nimekuuliza, kwa nini kaumba ulimwengu ambao unaruhusu mabaya, wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
Inaonekana hata wewe hujui jibu.
Unaamini Mungu ambaye humuelewi.
Huwezi kumuelewa.
Kwa sababu, hayupo. Ametungwa tu na watu.
Huwezi kumuelewa Mungu ambaye hayupo na habari za kuwapi kwake zinajipinga.
Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao watu wanatambua mema ila hauna na hauwezekani kuwa na mbaya?Utayajuaje mema bila kuyatambua mabaya?
Unaweza kuthibitisha ulimwengu huo usio na mabaya upo na si hadithi za uongo tu?Nimeshakujibu hili swali lako kwamba tayari ameuumba ulimwengu ujao usiokuwa na mabaya. Uwezo anao na ndio ameamua hivyo kwenye mali yake. Hakuna wa kumpangia.
Ungejuaje mema bila kuyatambua mabaya? au huoni hapo umepewa uhuru wa kuchaguaMungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao watu wanatambua mema ila hauna na hauwezekani kuwa na mbaya?
Mkuu me ningependa kujua wewe unaamini katika njia ipi/Mungu yupi maana vile unauliza maswali kuhusu Mungu ni kama vile huamini katika uwepo wake, ila cha ajabu ni kwamba wewe pia unaamini kuwa yupo, Naomba unisaidie kuelewa vile wewe unaamini juu ya uwepo wakeHiyo ina maana anaruhusu ubaya utokee, maana alimuona shetani kabla hajamrubuni mwanadamu, na bado akamuumba na kumpa uwezo mkubwa sana wakumrubuni mwanadamu. Halafu mwisho wa siku akamuadhibu mwanadamu akiyemuumba akijua atarubuniwa na shetani aliyemuumba yeye.
My head is spinning.
Anyway kwa kifupi mimi si kwamba siamini kama Mungi yupo, ila mimi nina imani yangu binafsi juu yake ambayo haifanani na ya dhehebu lolote.
Mabaya ni yapi? Unajuaje hili ni baya na hili ni zuri?Unaweza kuthibitisha ulimwengu huo usio na mabaya upo na si hadithi za uongo tu?
Mbona kama unataka kuthibitisha uongo mmoja ambao hauthibitishiki kwa kutumia uongo mwingine ambao hauthibitishiki?
Nakuuliza uthibitishe uwepo wa Mungu, unashindwa, unaleta habari za ulimwengu mwingine ambao hauthibitishiki.
Na kwa nini aruhusu mabaya kwenye ukimwengu huu?
Anapenda kuona mabaya yanavyoendelea?
Wewe unaongelea ulimwengu huu uliopo, ambao una mema na mabaya.Ungejuaje mema bila kuyatambua mabaya? au huoni hapo umepewa uhuru wa kuchagua
Mkuu,Hiyo ina maana anaruhusu ubaya utokee, maana alimuona shetani kabla hajamrubuni mwanadamu, na bado akamuumba na kumpa uwezo mkubwa sana wakumrubuni mwanadamu. Halafu mwisho wa siku akamuadhibu mwanadamu akiyemuumba akijua atarubuniwa na shetani aliyemuumba yeye.
My head is spinning.
Anyway kwa kifupi mimi si kwamba siamini kama Mungi yupo, ila mimi nina imani yangu binafsi juu yake ambayo haifanani na ya dhehebu lolote.
Mimi hata siendi kwa vipimo vyangu.Mabaya ni yapi? Unajuaje hili ni baya na hili ni zuri?
Nimeomba unipe metrics zitakazotumika kupima usahihi wa namna ya kuthibitisha uwepo wa Mungu na haujajibu.
Nyie atheist mnaamini kwenye kupasuka kwa utupu kwa bahati tu ndio ulimwengu huu ambao uko systematic and uniform ukatokea. Inashangaza mnapowazia evil and good wakati standard yenu ni bahati nasibu.Mkuu,
Kwa nini hii contradiction ya "the problem of evil" inayofanya kichwa chako kizunguke ni rahisi sana mimi na wewe kuiona, halafu watu wengine wengi wanakuwa kama hawaioni?
Ni uzembe wa kufikiri tu au nini?
Hujui hata atheism ni nini.Nyie atheist mnaamini kwenye kupasuka kwa utupu kwa bahati tu ndio ulimwengu huu ambao uko systematic and uniform ukatokea. Inashangaza mnapowazia evil and good wakati standard yenu ni bahati nasibu.
Nikupe mfano rahisi sana kuufikiria japo unaweza usiwe sahihi sana kumfananisha na alichofanya Mungu.Mimi hata siendi kwa vipimo vyangu.
Mimi nafanya "immanent critique".
Tuseme nakubaliana na wewe Mungu yupo (for the sake of argument, tupate sehemu ya kuanzia).
Na katika kukubaliana nawe hivyo, nakubaliana kwamba mambo ambayo kwa mujibu wa maelezo yako ya uwepo wa Mungu yamesemwa, ni kweli.
Kwa mfano, dhambi zipo na ni mbaya, kuua, kuiba, majanga, ni mambo mabaya.
Sasa nakuuliza, ili nipate kumuelewa vizuri huyu Mungu.
Mmesema huyu Mungu ana uwezo wote, ujuzi wote, upendo wote.
Kwa nini hakuumba ulimwengu huu uwe ambao mabaya hayawezekani, watu waishi na mazuri tu?
Ukijibu kuna ulimwengu huo mbinguni, hilo si jibu, mimi siulizi kama kuna ulimwengu usioruhusu mabaya, nauliza kwa nini hakuumba huu usiruhusu mabaya.
Mungu ambaye anaruhusu mabaya yasiyo idadi yaendelee miaka nenda rudi kwa kisingizio kwamba kuna ulimwengu unaokuja hautaruhusu mabaya atakuwa mkatili sana.
Ukisema katupa uchaguzi wa mabaya na mazuri, hilo si jibu, sijakataa kwamba katupa uchaguzi wa mabaya na mazuri, nauliza kwa nini kaachia mabaya yawezekane wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
Ulitaka ulimwengu wa aina gani?Siyo mimi ninavyotaka.
Ulimwengu ambao unawezesha watu kutwangana, unakanusha uwepo wa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.
Bado haujanijibu kwamba hao watu watajuaje wanayofanya ni mema wakati mabaya hawayatambui?Wewe unaongelea ulimwengu huu uliopo, ambao una mema na mabaya.
Mimi nakurudisha Mungu alivyokuwa anaumba ulimwengu, hakuna mema, hakuna mabaya, Mungu ndiyo anaamua jinsi ya kuumba.
Alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya, una mema tu na watu hawawezi kufanya mabaya, wanafanya mema tu.
Mungu alishindwa kuumba ulimwengu huo?
Ukiniukiza ningejuaje mema bila mabaya, una maana Mungu angetaka nijue mema bila mabaya kuwapo angeshindwa?
Kwa nini kutambua hili ni jema kuwe muhimu kuliko kufanya jema?Bado haujanijibu kwamba hao watu watajuaje wanayofanya ni mema wakati mabaya hawayatambui?
Kwanza kabisa, unaelewa kwamba, hapa, mjadala wangu si ninavyotaka mimi?Ulitaka ulimwengu wa aina gani?
Utajuaje umepika wali mbichi kama hujawai pika ulioiva?Kwa nini kutambua hili ni jema kuwe muhimu kuliko kufanya jema?
Unataka kuniambia kwamba, kati ya ulimwengu A ambao, watu hawajui jema ni lipi, kwa sababu hakuna mabaya, wanafanya mema tu, na ulimwengu B ambao watu wanatambua mema na mabaya, na wanafanya mabaya, ulimwengu B ni bora zaidi ya ulimwengu A?
Kwani Mungu ameshindwa kupika wali ulioiva bila kupika wali mbichi?Utajuaje umepika wali mbichi kama hujawai pika ulioiva?
Kwanza niambie kati ya ulimwengu A na B unaona sehemu gani wako huru zaidi..?